Posts

Showing posts from June 12, 2015

WAZIRI MKUU MH. MIZENGO PINDA ACHUKUA FOMU ZA KUWANIA UTEUZI WA CCM KUGOMBEA URAIS

Image
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitia saini kitabu baada ya kuwasili kuwasili kwenye Ofisi Kuu ya CCM mjini Dodoma kuchukuwa fomu za kuwania uteuzi wa CCM ili awe mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao . Kulia ni Mkewe Tunu na kushoto ni Katibu wa Nec CCM, Mohammed Seif Khatib. Waziri Mkuu , Mizengo Pinda akiwa ameshika fomu ya kuwania uteuzi wa CCM ili awe mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao kwenye ofisi kuu ya CCM mjini Dodoma Juni 12, 2015. Kulia ni Mkewe Tunu na kushoto ni Katibu wa Nec CCM, Mohammed Seif Khatib. Waziri Mkuu , Mizengo Pinda akizungmza na waandishi wa habari na wananchi waliofika kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM mjini Dodoma kushuhudia wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipochukuwa fomu ya kuwania uteuzi wa CCM ili awe mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao kwenye ofisi kuu ya CCM mjini Dodoma Juni 12, 2015. Baadhi ya waandishi wa habari na wananchi waliofika kwenye ukumbi wa Halmash...

URAIS CCM KAZI IPO

Image

LOWASSA AZIDI KUVUNJA REKODI YA WADHAMINI, APATA 9516 MKOANI TABORA LEO

Image
Waziri Mkuu wa Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wana CCM waliofika kumdhamini pamoja na wananchi wengine, kwenye viwanja vya ofisi za CCM Tabora Mjini, leo Juni 12, 2015. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wana CCM 9516 kwa mkoani Tabora, ikiwa ni muendelezo safari yake ya kutafuta wana CCM wa kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi kimteue kuwania nafasi ya urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI. Waziri Mkuu wa Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akipokea majina kutoka kwa Naibu Katibu wa CCM Wilaya ya Tabora Mjini, Bi. Hidaya Rashid yenye idadi wanachama wa CCM 9516 waliomdhamini ili aweze kuteuliwa na Chama kuwania Urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Waziri Mkuu wa Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akizungumza na WanaCCM waliofika kumdhani pamoja na wananchi wa Mj...

WAZIRI BERNARD MEMBE ANUSURIKA AJALI YA NDEGE, ZANZIBAR

Image
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (pichani) , amenusurika kifo baada ya ndege aliyokuwa akisafiria kutoka Iringa kwenda Zanzibar kutaka kugongana uso kwa uso na ndege nyingine dakika moja kabla ya kutua. Waziri Membe akiwa na ujumbe wake wa watu wanane, walikuwa wakisafiria ndege ya kukodi kampuni ya 5H NEG Precition Aviation ikirushwa na rubani Mathew Mhahiki, ambaye ameonyesha kushangazwa na tukio hilo alilodai “ni kwa rehema za Mungu tumepona ajali hii.”  Akizungumza na mwandishi wetu aliyeko katika ziara yake, rubani Mhahiki alisema: “Lazima kuna tatizo katika control center hata hivyo tayari nimeongea nao na wameniomba samahani na kudai walipitiwa, maana kwa hali ilivyokuwa ni kwamba tungegongana wakati wa kutua maana nimeshangaa tu kuona ndege hii hapa ndiyo maana nikaamua kumkwepa mwenzangu nikapanda juu.” Waziri Membe alisema: “Nina uzoefu mkubwa wa kusafiri na ndege mahali peng...

JINSI SITTI MTEMVU ALIVYOYABADILISHA MAUMIVU YA SIKU 30 KUWA BIASHARA

Image
Aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Uingereza kuanzia mwaka 1940 hadi 1945 na kisha kurejea tena mwaka 1951 hadi 1955, Winston Churchill aliwahi kusema, “a pessimist sees the difficulty in every opportunity; an optimist sees the opportunity in every difficulty.” Alimaanisha kuwa “mtu muoga huona ugumu kwenye kila fursa na mtu jasiri huona fursa kwenye kila ugumu.” 2014 ulikuwa ni mwaka wenye majaribu na mitihani mingi kwa Sitti Mtemvu. Mara tu baada ya kushinda taji la Miss Tanzania 2014, skendo moja baada ya nyingine zikaanza kuibuka. Kubwa lilikuwa ni kitendo chake cha kudaiwa kudanganya umri na kuwasilisha cheti cha kuzaliwa ‘feki.’ Pia watu wakazusha kuwa mrembo huyo ana mtoto, kitu ambacho ni kinyume cha vigezo vya shindano hilo lililofungiwa mwaka jana. Sitti alijikuta kwenye kitimoto. Jina lake likavuma mitaani, kwenye vyombo vya habari na zaidi kwenye mitandao ya kijamii. Habari yake ya kudanganya umri ikawa kubwa kuliko ushindi wenyewe wa taji hilo. Watu...

WASHINDI TUZO ZA KILI KUANIKWA KESHO

Image
Meneja wa Kilimanjaro ,Pamela Kikuli akizungumza na wanahabari (hawapo)pichani. Wanahabari wakichukua tukio. WASHINDI wa Kilimanjaro Music Awards 2015 (KTMA) wanatarajiwa kuanikwa kesho ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar. Akizungumza na waandishi wa habari leo, Meneja wa Kilimanjaro, Pamela Kikuli amesema kuwa washindi waliopatikana katika Promosheni za Bia ya Kilimanjaro zilizofanyika nchini kote wameanza kuwasili jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo kushuhudia Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards. “Hafla ya kukabidhi tuzo hizi inategemewa kufanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kesho Jumamosi na jumla ya washindi 22 wanatarajiwa kuwasili leo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania ambapo washindi hawa wataungana na washindi wengine wanne wa hapa Dar es Salaam,” alisema Kikuli. Bi. Pamela aliongeza kuwa washindi hao waliochaguliwa kwa njia ya kuponi baada wanywaji kununua bia ya Kilimanjaro kwenye Bar zilizokuwa na Promosheni watalipiwa ...

OFFICIAL : MAN UNITED YAKAMILISHA USAJILI WA MEMPHIS DEPAY NA KUMPA JEZI

Image
Klabu ya Manchester United imetangaza  rasmi kukamilisha usajili wa nyota wa kimataifa wa Uholanzi,  Memphis Depay na kumsainisha mkataba wa miaka minne. Mpango wa kumsajili kinda huyu mwenye miaka 21 ulikamilika mwezi uliopita, lakini sasa dili limekamilika rasmi ambapo United imelipa ada ya uhamisho ya  paundi milioni 25. Kiungo huyo anajiunga na Manchester United kutokea klabu ya PSV Einhoven ambapo alionesha kiwango cha juu kwenye ligi ya Uholanzi akifunga magoli 22 msimu uliopita. Kijana huyo pia ameonesha kiwango kizuri timu ya taifa na wiki iliyopita alicheza mpira mwingi mno Uholanzi ikifungwa 4-3 na Marekani. Memphis Depay anakuwa mchezaji wa kwanza  kusajiliwa rasmi na Man United majira haya ya kiangazi ambapo Louis van Gaal anatafuta wachezaji wa kuimarisha kikosi cha kushindania ubingwa msimu ujao.

DAKTARI: KAJALA HAWEZI KUZAA TENA!, KISA HIKI HAPA

Image
Imelda mtema MAJANGA juu ya majanga! Siku chache kufuatia kufanyiwa kipimo na kubainika kuna tatizo kwenye ubongo baada ya kupigwa chupa kichwani kwenye Klabu ya New Maisha, Masaki jijini Dar, mkali wa sinema za Bongo, Kajala Masanja ‘Kay’ amepata pigo lingine la daktari kumwambia hawezi kuzaa tena!   Mkali wa sinema za Bongo, Kajala Masanja ‘Kay’. Kwa mujibu wa chanzo makini, Kajala alipewa maelezo hayo mapema wiki hii baada ya kufanyiwa kipimo na daktari bingwa wa hospitali moja iliyopo maeneo ya Morocco jijini Dar. HISTORIA YA TATIZO Kwa mujibu wa chanzo hicho, awali staa huyo alikuwa akisumbuliwa na tatizo la maumivu makali ya tumbo kwa kipindi kirefu na mara kwa mara hali iliyomlazimu kwenda kwenye hospitali mbalimbali za jijini Dar na kutibiwa lakini bila mafanikio. “Unajua awali, aliamini amepata vidonda vya vitumbo (Ulcers). “Pamoja na kupewa dawa mbalimbali kama ‘antibiotic’ kama Amoxicillin, Tetracycline, Clarithromycin na Metronidazole,...

UZINDUZI WA BONGO STAR SEARCH 2015 “JUKWAA LAKO- KUWA ORIGINAL”

Image
…akizindua awamu nyingine ya shindano la BSS kwa mwaka 2015. Kushoto ni Madam Rita, kabla ya uzinduzi akiwa na mmoja wa wadau, kulia ni mbunifu wa mitindo nchini Ally Remtullah. Mmoja wa washindi wa BSS mwaka 2013, Emmanuel Msuya akizungumza jambo na wanahabari (hawapo pichani). Baadhi wa waandishi wa habari wakifuatilia kipindi maalumu cha wasanii na washindi waliopita katika shindano la BSS, miaka ya nyuma. Sehemu ya waraka kwa Watanzania.