Posts

Showing posts from May 26, 2017

Wolper Atokwa na Povu Baada ya Kubanwa Kuhusiana na Madai ya Kunuka Mwili

Image
Staa wa filamu ‘grade one,’ ‘Jacqueline Wolper’. STORI: ALLY KATALAMBULA NA BONIPHACE NGUMIJE, IJUMAA , HABARI Staa wa filamu ‘grade one,’ ‘Jacqueline Wolper’ ametokwa povu si la nchi hii baada ya kubanwa kuhusiana na madai ya kunuka mwili na kusema hajawahi kunuka maishani mwake na kwamba ingekuwa hivyo asingepapatikiwa na wanaume. Hivi karibuni Ijumaa lilimfungia kazi msanii huyo nyumbani kwake na katika moja ya maswali aliyobanwa lilikuwa juu ya ishu iliyosambaa kuwa eti anatoa harufu mbaya sehemu za mwili wake. Katika kuonesha kumaindi ile mbaya kuhusu madaia hayo, mrembo huyo ambaye kiukweli yuko bomba kwa muonekano alifunguka: “Aliyekuambia nanuka nani? Mimi sinuki wala sijawahi kunuka maishani mwangu, kuthibitisha hilo kwanza nisingekuwa napapatikiwa na wanaume kila kukicha sambamba na kuhongwa vitu kibao huku wengine nikiwaacha wakinililia. Hao wanaosema na kusambaza hayo ni njia tu ya kujipatia followers kwenye mitandao yao kupitia mimi.” Wolp

Polepole: Watu wanaishi kwa hofu

Image
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amefunguka na kusema watu wamekuwa na hofu huku wengine wakihama makazi yao mkoani Pwani kutokana na vitendo vya mauaji vinavyoendelea mkoani humo. Polepole amesema wao kama CCM wanaitaka serikali ichukue hatua za haraka katika jambo hilo kwa kuwa ina vyombo vyote vya ulinzi na usalama, hivyo wanataka kuona jambo hilo linapewa umaalum katika kulishugulikia. "Sisi kama chama tumelifuatilia hili suala kwa umakini sana na tumeona ni vyema kusimama na Watanzania wakiwepo na wanachama wa CCM wa maeneo haya, tunatambua wanapitia wakati mgumu sana kwani wapo viongozi wetu, wapo wanachama wa CCM, na watendaji mbalimbali wamepoteza maisha. Wamepoteza maisha si kwa sababu ya mapenzi ya Mwenyezi Mungu bali maisha yao yamekatizwa kikatili" alisisitiza Polepole Kufuatia mambo haya kuendelea kutokea mkoani Pwani Chama Cha Mapinduzi kimetoa salamu za pole kwa wananchi wote ambao wameguswa na misiba ya watu am

Faida (6) za tangawizi

Image
Siku kadhaa zilizopita tuliona kwa uchache faida za tangawizi, naomba siku ya leo tuendelee faida nyingine za tangawizi ambazo ni; 1. Husaidia wenye kifafa au Msongo wa mawazo Wataalamu wanasema kifafa kinasababishwa na mishipa kuvimba na kukandamiza ubongo na tangawizi inatumika husaidia kuondoa mafuta katika mishipa, kutia joto mwili na kusaidia damu yenye oxygen kusambaa mwilini na kwenye ubongo bila shida. 2. Huondoa gesi tumboni Tangawizi husaidi mmeng'enyo wa chakula tumboni, kwa hiyo husaidia matatizo mengi yanayosababishwa na ulaji. 3. Husaidia kutibu mafua, kikohozi Unachitakiwa kufanya. Changanya mdalasini, pilipili manga kidogo, chemsha kama chai pamoja na tangawizi. Husaidia sana mafua na kikohozi. 4. Huongeza nguvu za kiume Tangawizi inauwezo wa kuongeza joto mwilini, hivyo huamsha mishipa ya fahamu katika mwili wa mwanaume mwenye tatizo hilo. 5.Huongeza maziwa kwa kina mama wanyonyeshao. Kwa kina mama wanaonyenyesha tangawizi inachoche

NAIBU WAZIRI DKT.KINGWANGALLA AMTEMBELEA MZEE MAIGE’NGOSHA ‘ MUHIMBILI

Image
Naibu Waziri Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kingwangalla akiongea na Mzee Maige ambaye amelazwa kwenye chumba cha kitengo cha dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo asubuhi ya leo mzee huyo alihamishiwa hapo kwa uchunguzi wa afya na matibabu zaidi kutoka hospitali ya Rufaa ya Amana. Daktari Bingwa wa magonjwa ya dharura Renatus Tarimo(kushoto) akimueleza Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto jinsi walivyompokea na kumuhudumia kwenye kitengo chao na hali ilivyo hadi sasa,Dkt. Tarimo amesema hali ya Mzee maige inaendelea vizuri na wameshamfanyia uchunguzi wa awali na wanaendelea na uchunguzi zaidi Mkuu wa Kitengo cha Dharura Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga (katikati) akimueleza jambo Naibu Waziri Dkt. Kingwangalla mara baada ya kutoka kwenye chumba alicholazwa Mzee Maige.Mzee Maige au kwa jina maarufu anajulikana kama Ngosha ndiye aliyebuni Nembo ya Taifa ambayo ina