Uchaguzi Zanzibar; Dk Shein, Balozi Seif wapiga kura zao
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. Ali Mohamed Shein akipiga kura katika uchaguzi wa marudio kituo cha kupiga kura namba 1 Skuli ya msingi Bungi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo, Wananchi wa Zanzibar leo wanapiga kura katika uchanguzi wa marudio baada ya kufutwa kwa uchanguzi uliofanyika Oktoba 25, 2015 kutokana na kasoro zilizojitokeza. Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi akiwa katika maandalizi ya kupiga kura katika uchaguzi wa marudio kituo cha Skuli ya Kitope, Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini. Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi akipiga kura katika uchaguzi wa marudio kwenye kituo cha Skuli ya Kitope, Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini. Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi akizungumza na baadhi ya Waandishi wa Habari mara baada...