Mbasha akiwa na Pingu. WAKATI mume wa mwimba Injili Bongo, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha akiachiwa huru kwa dhamana kufuatia kesi ya kudaiwa kumbaka shemejiye, Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la jijini Dar es Salaam, Josephat Gwajima ameibuka na kunena mazito kuhusiana na sakata hilo, Risasi Jumamosi limesheheni mkobani. Mbasha aliachiwa kwa dhamana juzi akitokea Gereza la Keko, Dar baada ya kupandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Juni 17, mwaka huu na kusomewa mashitaka mawili ya ubakaji ambayo hata hivyo, aliyakana. Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la jijini Dar es Salaam, Josephat Gwajima. ILIVYOKUWA KORTINI Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, mheshimiwa Wilbeforce Luago siku hiyo ya Juni 17, alitoa hoja kwamba upande wa jamhuri hauna pingamizi hivyo dhamana ipo wazi. Emmanuel Mbasha akielekea kizimbani. Alisema mshitakiwa alitakiwa kuwa na wadhamini wawili, m...