Hatimaye Mtatiro ‘Amchana’ Prof. Lipumba, Amuita ni Jemedari Aliyekimbia Vita
Dar es Salaam: Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro amesema aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba amekiacha chama kwenye wakati mgumu baada ya kujiuzulu wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2015. Agosti, mwaka jana, Profesa Lipumba alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kukabidhi barua kwa uongozi baada ya kushauriana kwa kipindi kirefu na viongozi na wazee wa chama hicho, akisema nafsi yake inamsuta kwa kuwa walikiuka malengo ya Ukawa. Hata hivyo, hivi karibuni Profesa Lipumba aliandika barua ya kutengua uamuzi wa kujiuzulu na uchaguzi ulipoitishwa ili kujaza nafasi hiyo hakuchukua fomu ya kugombea. Akizungumza katika mahojiano maalumu, Mtatiro amesema Profesa Lipumba amekitelekeza chama kikiwa katikati ya uwanja wa mapambano. Mtatiro aliyeteuliwa hivi karibuni na Baraza Kuu la CUF kuongoza kamati ya uongozi wa chama hicho baada ya kuvunjika kwa mkutano mkuu ulioitishwa kuziba nafasi ya mwenyekiti, amesema walijaribu kila mbin...