HIKI NDIO CHANZO kuhusu kupigwa risasi kwa mtangazi wa ITV ( Ufoo Saro ) ambaye mama yake naye AMEFARIKI
Alfajiri ya leo, mtangazaji wa ITV anayejulikana kwa jina la Ufoo Saro amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi na mchumba wake ambaye baada ya tukio hilo naye alijipiga risasi na kujiua. Akizungumza na mpekuzi wetu, kamanda Wambura ambaye ni kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa kinondoni amesema tukio hilo limetokea majira ya alfajiri ya leo. Kamanda wambura amedai kuwa mwanaume aliyetenda mauaji hayo ni mchumba wake na alikuwa anafanya kazi katika umoja wa mataifa ( UN ) huko sudani ila bado haijafahamika kitengo alichokuwa akifanyia kazi. Kwa mujibu wa Kamanda Wambura, inasemekana kulikua kuna ugomvi kati ya wawili hao ambapo walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi wa Ufoo Saro(mama mkwe) ili awasuluhishe Baada ya usuluhishi kuanza na kuonekana kuwa tatizo liko kwa mwanaume, mwanaume huyo alimshutumu mama mkwe wake kwamba amekuwa na mazoea ya kumtetea mwanae na ndipo alipotoa bast...