Posts

Showing posts from May 5, 2016

HATIMAYE Snura awaomba radhi Watanzania, awasilisha video safi ya Chura kukaguliwa

Image
Snura amewaomba radhi watanzania kwa video ya wimbo wake ‘Chura’ inayowadhalilisha wanawake na iliyo kinyume na maadili. Snura akiongea na waandishi wa habari Alhamis hii Muimbaji huyo amekutana na waandishi wa habari Alhamis hii kwenye ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam. Jana video na wimbo huo vilifungiwa na wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo kwa madai kuwa inakiuka maadili ya Kitanzania. Pia alizuiwa kufanya maenesho ya hadhara kwakuwa hajajisajili kwenye baraza la sanaa la taifa, BASATA. Kwenye mkutano huo na waandishi wa habari, Snura amedai kuwa tayari amekamilisha mchakato wa usajili na BASATA imempa kibali. Pia amedai kuwa amewasilisha video mpya ya wimbo huo kwa bodi ya filamu ya Tanzania ambayo itaikagua.

Kikwete 'Agoma' Kumkabidhi Rais Magufuli Chama......Mwinyi,Mkapa,Malecela Kukutana kwa Dharura Kumjadili

Image
Hali si shwari ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na mchakato unaoendelea wa kumkabidhi Rais Dk. John Magufuli uenyekiti wa chama hicho, kukumbwa na sintofahamu. Taarifa kutoka ndani kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC), kilichofanyika juzi Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma, zimethibitisha kutokea mgawanyiko wa vigogo ndani ya chama hicho. Hali hiyo imekuja baada ya kutokea kwa mvutano juu ya tarehe rasmi ya kufanyika kwa mkutano mkuu maalumu uliopangwa Juni mwaka huu, ambao pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Rais mstaafu Jakaya Kikwete atakabidhi kijiti kwa Rais Magufuli. Chanzo cha kuaminika ndani ya kikao hicho kilidokeza  kuwa, kabla kilifanyika kikao kidogo kilichokuwa na wajumbe wanne ambao pamoja na mambo mengine walijadili ajenda muhimu  ikiwamo ya kupanga tarehe kwa ajili ya mkutano huo. Kwa mujibu wa chanzo hicho, kikao hicho kidogo kilishirikisha viongozi wanne akiwemo Mwenyekiti wa chama hich...

REAL MADRID WAICHAPA MAN CITY KWA BAO 1-0 NA KUTINGA FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA

Image
Real Madrid imefanikiwa kufuzu kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayochezwa Mei 28 jijini Milan, Italia. Madrid imetinga fainali baada ya kuitwanga Man City kwa bao 1-0 katika mechi ya pili ya nusu fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid. Bao la Madrid limepatikana baada ya shuti la Gareth Bale aliyekuwa akipiga krosi kumgonga Fernando na kujaa wavuni. Pamoja na Madrid kutinga fainali, maana yake Kocha Zinedine Zidane ameandika rekodi yake ya kwanza kucheza fainali hiyo, safari hii akiwa kocha. Lakini Man City imeishia nusu fainali iliyokuwa ni mara ya kwanza kwake kuingia Ushindi huo wa bao 1-0, unaipitisha Madrid hadi fainali baada ya sare ya bila bao katika mechi ya kwanza jijini Manchester.

Mauaji ya Kutisha Kaole Bagamoyo Jana Jioni..Mama na Mtoto Wachinjwa Kama Kuku

Image
TAARIFA YA MAUAJI.BAG/IR/1078/2016.MNAMO 04/05/2016 MAJIRA YA SAA 16.30HRS HUKO KAOLE KWENYE VICHAKA KATA YA DUNDA (W)B'YO(M)PWANI OLVER S/O ERASTO,22YRS,MCHAGA,MKULIMA, WA KAWE DSM NA MTOTO WAKE EMMANUEL S/O FROWIN PETER,3YRS MHEHE WOTE WALIUAWA KWA KUCHINJWA SHINGONI KWA KUTUMIA KISU NA MME WAKE FROWIN S/O PETER,MBWALE,26YRS,MHEHE,DEREVA,MKAZI WA KAWE DSM AKISHIRIKIANA NA RAFIKI YAKE RAJABU S/O JUMA,20YRS,MKULIMA,MKAZI WA MAKONGO DSM.MIILI YAO IMEKUTWA UMBALI WA MITA 100 KUTOKA BARABARANI.CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI WIVU WA MAPENZI AMBAPO MUME WA MAREHEMU ALIMUHISI KUWA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA MTU AITWAYE HAMZA S/O ? MKAZI WA KAWE DSM .MBINU ALIMDANGANYA KWAMBA WAODOKE PAMOJA NA MTOTO WAO KWENDA KAOLE BAGAMOYO KUANGALIA NYUMBA YAO ANAYOENDELEA KUJENGA WALIKODI PIKIPIKI MC 235 AWR FECON HADI KAOLE PORINI.WATUHUMIWA WAMEKAMTWA NA WAMEKIRI KUFANYA MAUAJI HAYO = Samahani kwa Kuficha Picha , Sio Nzuri Watu wawili mama na mtoto wamenyongwa hadi kufa ki...