Posts

Showing posts from January 17, 2016

UKAWA WASHINDA KITI CHA UMEYA MANISPAA YA ILALA.

Image
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kwiyeko akizungumza na madiwa wa Manispaa ya Ilala leo mara bada ya kushinda  kwa Kura 31 katika uchaguzi wa meya wa manispaa hiyo katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam. Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Salum Kumbilamoto  akiwashukuru madiwani waliompigia kura leo mara ya kuibuka kidedea katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya  wapiga kura wakipiga kura za Meya na Naibu leo katika uchaguzi  wa kuwapata viongozi hao wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam. Matokeo ya Meya na Naibu Meya yakujumlishwa na baadhi ya wajumbe wa Meya,naibu Maya  wakiwa na Mwanasheria wao leo mara baada ya kumaliza kugika kura katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.  Baadhi ya viongozi wakiwa kwenye ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya...

HATUA AMBAZO ZIMECHUKULIWA DHIDI YA STANBIC BANK TANZANIA LIMITED KUHUSU USHIRIKI WAKE KUWEZESHA MKOPO WA SERIKALI WA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 600

Image
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Mpango (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawamo pichani)jijini Dar es Salaam, kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali dhidi ya Benki ya Stanbic Tanzania kutokana na ushiriki wake katika kuwezesha mkopo wa Serikali wa Dola za Kimarekani Milioni 600 na Kulia kwake ni Naibu Gavana  wa Benki Kuu ya Tanzania(BOT) Bw. Lila Mkila. Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Mpango (katikati)  akitoa tamko kwa waandishi wa habari (hawamo pichani) jijini Dar es Salaam, kuhusiana na kusudio la kuitoza Benki ya Stanbic faini ya shilingi bilioni 3.  Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servicius Likwelile na Kushoto kwake ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Lila Mkila. ……………………………………………………………………………………… Utangulizi Mwezi Julai 2013, Benki Kuu ya Tanzania kupitia ufuatiliaji wa kawaida wa shughuli za mabenki iligundua matatizo yaliyohusia...