Posts

Showing posts from November 11, 2018

Jinsi yakumtambua mpenzi wako kama anamapenzi ya dhati kwako

Image
Watu wengi huwa wanajiuliza sana swali hili,nitamjuaje kama mpenzi wangu ananipenda kweli,swali hili huwa ni gumu sana kwa watu wengi,lakini minapenda kulijibu leo kama ifuatavyo; Hapa duniani kuna mapenzi ya aina mbili(selfish love and unselfish love)mapenzi ya uchoyo na mapenzi yasio ya uchoyo,mapenzi ya uchoyo ni yale mapenzi ambayo mpendwa mmoja wapo hupenda kupendwa yeye tu kujaliwa yeyetu, pasipo kurudisha upendo kwa mwenzie vile inavyotakiwa kwa lugha nyingine mtu mwenye mapenzi ya uchoyo huwa sio mbunifu katika kupendezesha penzi na mara nyingi huwa ni mtu mwenye lawama na ambae haridhiki kwa kila jambo zuri atakalofanyiwa,(unselfish love)mapenzi yasiyokuwa ya uchoyo haya ndio mapenzi ya kweli,watu wenye mapenzi ya kweli huwa wanapenda kutoa kuliko kupewa na pia hutoa pasipo kuwa na matarajio ya kupata kitu flani. Bali kutoa kwao ndio furaha ya moyo wao,kama ni mwananke anakuwa anamjali sana mpenzi wake pale anapokuwa na vijisenti kidogo akiona shati ama

MREMBO SUDAN AOLEWA KWA NG’OMBE 520, TOYOTA 3 KALI

Image
Nyalong na mumewe Kok Alat siku ya ndoa. HATIMAYE familia ya mrembo wa Sudan ya Kusini aliyekuwa anagombewa na waposaji kibao walioahidi kutoa mahali kubwa zisizo za kawaida, imepokea mahari ya ng’ombe 520 na magari matatu aina ya Toyota V8 baada ya binti yao kuolewa! Mrembo Nyalong Ngong Deng (17) kutoka eneo la Awerial, alikuwa na wachumba sita waliokuwa wanamtaka na kila mtu alikuwa tayari kutoa mahali bab’kubwa ikiwa ni pamoja na Sh. milioni moja za Kenya ambazo ni sawa na Sh. milioni zipatazo 20 za Tanzania! Akiwa amekaa kwa utulivu kando ya mumewe, tajiri mkubwa aitwaye Kok Alat katika ukumbi wa Freedom Hall jijini Juba, Ijumaa iliyopita, Novemba 9, Nyalong, mrembo wa kabila la Dinka,  alikuwa nadhari ya mshangao uliowapata watu waliokuwa katika sherehe hiyo. Nyalong akiwa nyumbani kwao; na baba na nduguze kabla ya ndoa. Nyalong, mumewe.

NYUMBA ALIMOFICHWA ‘MO’ YAFAHAMIKA, NI MBEZI BEACH DAR

Image
Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, akiongea na waandishi wa habari leo. NYUMBA inayodaiwa kuwa ndimo alifichwa mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo’ baada ya kutekwa na watu ambao bado hawajajulikana hadi leo ipo eneo la Mbezi-Beach jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, ameonyesha nyumba hiyo ambayo watekaji hao waliikodisha kwa kupanga kwa kusaidiwa na mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la Twalib Mussa.Kwa mujibu wa maelezo ya Mambosasa, kufuatana na uchunguzi uliofanywa kwa kumhusisha pia Twalibu, watekaji hao walitoka  Afrika Kusini. Mohammed Dewji ‘Mo”. Mambosasa alisema kupatikana kwa nyumba ambayo ilikuwa inamilikiwa na mtu mmoja marehemu aliyemtaja kwa jina la Mwansasu, ni moja ya hatua muhimu katika sakata hilo lililoanza kwa kutekwa kwa mfanyabiashara huyo kijana siku ya Oktoba 11 mwaka huu ambapo leo umetimia mwezi hadi kupatikana kwa nyumba aliyokuwa amet

Tamasha la Tigo Fiesta laacha gumzo jijini Arusha

Image
Msanii Maua Sama anayetamba na kibao chake cha Iokote akitoa burudani ya aina yake kwa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya walioshiriki katika tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018. Wasanii wanaounda kundi la Weusi wakiongozwa na Joh Makini wakiwapagawisha mamia ya mashabiki walioshiriki katika tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika katika uwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha mwishoni mwa wiki. Msanii Rich Mavoko akitoa burudani kwa maimia ya mashabiki waliofurika katika Tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018. Msanii Whozu na madensa wake wakitumbuiza katika Tamasha la Tigo Fiesta 2018 lilofanyika katika kiwanja cha  Sheikh Amri Abeid jijini Arusha mwishoni mwa wiki. JIJI la Arusha, jana lilishuhudia show za kufunga mwaka zilizojaa ubunifu na vituko vya aina yake kutoka kwa wasanii mbali mbali waliopanda jukwaani kutumbuiza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyilka katika  uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Msanii Whozu alikuwa ni kivutio kikubwa