Posts

Showing posts from August 20, 2017

GAVANA SONKO AAMUA KUMUIGA RAIS MAGUFULI

Image
Gavana mteule wa jimbo la Nairobi nchini Kenya Mike Sonko, ameingia kitendo cha Rais Magufuli alichofanya baada ya kuingia madarakani cha kuingia mtaani na kufanya usafi, huku akiweka kampeni maalum ya usafi. Kwenye ukurasa wake wa instagram Mike Sonko ameweka picha na kuandika kuwa serikali yake itasimima suala hilo ili kuweka mji safi, ili kutunza mazingira na kujiepusha na magonjwa ya kumbukiza. “Ni muhimu kwetu kujua na kuweka mazingira safi kwani muhimu kwa maisha yetu, na serikali yangu itawezesha kila kinachohitajika ili kufanya usafi, ili kuonyesha dhamira yetu tumetoa mapipa ya kutunzia takataka 20, mikokoteni 10, koleo 10, reki 10, viatu, mipira ya mikono na vitu vingine kwa kila kata hapa Nairobi, kwa kazi za kawaida:”, aliandika Sonko. Sonko aliendelea kuandika “Tukitaka kuondokana na kipindu pindu a magonjwa mengine mabaya, tunahitaji kuweka mazingira yetu safi, nahimiza kuacha kutupa taka hovyo, tutumie hivi vifaa ipasavyo

SIMBA WAKUTANA KUMPA TIMU MO DEWJI

Image
Wanachama wa Klabu ya Simba wakijiandaa kwa ajili ya mkutano huo. Kwa mara nyingine tena, Wanachama wa Klabu ya Simba wamekutana kufanya Mkutano Mkuu wa Klabu leo Jumapili kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyarere International Conference Centre) jijini Dar es Salaam. Maanadalizi ya ya mkutano huo. Ukumbi huo wa kisasa kabisa nchini upo maeneo ya Ocean Road, jirani na Chuo cha Usimamizi wa fedha (IFM), utakuwa unatumiwa kwa mara ya pili na klabu hiyo baada ya kutumika Jumapili iliyopita. Wanachama wakijadiliana kabla ya mkutano huo. Mkutano huo ni mwendelezo wa maandalizi ya Klabu ya Simba kufanya mabadiliko ya kimfumo katika kuiongoza klabu hiyo. Msemaji wa Simba, Haji Manara akizungumza. Mmoja wa wanachama maarufu wa Simba, Mohamed Dewji ‘MO’ anatarajiwa kuwa mmoja wa wadau waliopanga kuwekeza baada ya mfumo wa uendeshaji kubadilishwa. Hali ilivyo ukumbini hapo.   Wanachama ni furaha kwenda mbele. PICHA NA MUSA

KENYA: Odinga Auawa, Mwili Wake Watupwa Sokoni

Image
Caroline Odinga enzi za uhai wake. JESHI la Polisi katika Kaunti ya Siaya linaendelea na upelelezi baada ya mwili wa mwalimu wa kike aliyetambulika kwa jina la Caroline Odinga ambaye alikuwa msimamizi msaidizi wa Tume ya Uchaguzi (IEBC) katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya wa Agosti 8 mwaka huu. Mwili wa mwalimu huyo wa Ugenya High School ulikutwa katika soko la Sega jana Jumamosi asubuhi na watu waliokuwa wakielekea katika mazishi ya Mkurugenzi wa TEHAMA wa IEBC, Chris Msando, Kijiji cha Lifunga. Soko ambapo mwili wake umekutwa. Mkuu wa Polisi katika Kaunti ya Siaya, Sarah Duncan amesema uchunguzi unaendelea na upelelezi wa awali unaonyesha kuwa marehemu alibakwa na watu wengi na sehemu zake za siri pamoja na sikio moja kukatwa vibaya. Familia yake inaeleza kuwa mara ya mwisho alitoka nyumbani siku ya Ijumaa na kwenda kudai malipo yake kwa kazi aliyofanya ya usimamizi wa Uchaguzi Mkuu uliomalizika.

DAR: Wapigadebe 150 Watiwa Mbaroni

Image
Picha na maktaba. Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limetangaza kukamata watu wapatao 150 kuanzia Agosti 14 hadi 17 mwaka huu, kwa makosa ya kuwabughuzi abiria katika maeneo mbalimbali ya jiji katika vituo vya mabasi. Wakati akizungumza na wanahabari jana  jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda Lucas Mkondya, alisema watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia misako na operesheni kali iliyofanywa na polisi, na kwamba watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili. “Stendi ya mabasi ya Ubungo walikamatwa 39, Posta 12, Ferry 7, Tegeta 12, Tandika 16, Mnazimmoja 6, Stesheni 5, Manzese 12, Bunju 8 na Stereo 7,” amesema. Katika hatua nyingine, Kamanda Mkondya alisema Jeshi la Polisi katika nyakati tofauti ilikamata watuhumiwa 167 kwa makossa mbalimbali ya kihalifu ikiwemo kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, unyang’anyi wa kutumia sialaha na utapeli, kucheza kamali na kuuza pombe haramu ya gong