Mgombea Ubunge ‘Aliyetekwa’ Mtwara Apatikana.......Ndugu Wasimulia Tukio Zima, Polisi Wasema Wanachunguza Kama Ni Kweli Au Lilipangwa
Mgombea ubunge jimbo la Mtwara Mjini kupitia CHADEMA, Joel Nanauka alipotea katika mazingira ya kutatanisha tangu juzi na kukutwa ametupwa nje ya mlangoni wa jengo la Kliniki/kituo cha afya hapo Mtwara. Ndugu wa mbunge huyo wameusimulia mkasa huo kama ifuatavyo: "Ndugu yetu Joel Nanauka ambaye anagombea Ubunge Jimbo la Mtwara Mjini kupitia CHADEMA, alipotea katika mazingira ya kutatanisha siku ya Jumatatu Tarehe 5/10/2015. Siku hiyo alitoka kwenye shughuli za kampeni akiwa na wenzake na walirudi nyumbani akiwa amechoka. "Majira ya saa kumi na mbili na nusu, alimtumia mwenzake ujumbe mfupi wa mkononi (SMS) akimjulisha kwamba kuna mtu amekua akimtafuta tangu wiki iliyopita waonena na mchana wa siku hiyo alimfuata ofisi ya CHADEMA lakini hakumkuta, hivyo anakwenda kuonana naye mara moja eneo linal...