Posts

Showing posts from October 17, 2015

Maneno Ya Lowassa jinsiAlivyopokea Kifo Cha Filikunjombe

Image
Ni taarifa ya kushtusha sana ya msiba wa mwanasiasa chipukizi na jasiri, Deo Filikonjombe kutokana na ajali ya Helikopta jana jioni maeneo ya mbunga ya Selous mkoani Morogoro. Ni pigo lingine kubwa ambalo katika kipindi kifupi Taifa limepata, huku bado likiwa na kidonda cha kuondokewa na wana siasa wengine mahiri,Marehemu Celina Kombani, Dr Abdallah Kigoda na Dr Emanuel Makaidi aliyefariki jana Filikonjombe alikuwa Mbunge mahiri aliyesimama imara kutetea maslahi ya wananchi wa jimbo lake la Ludewa na watanzania kwa ujumla. Alikuwa mwiba kwa serikali ya Chama chake CCM kutetea maslahi ya nchi, mfano ni katika kashfa ya Escrow ambapo alikuwa Makamu Mwenyekiti wa kamati iliyochunguza kashfa hiyo. Mwenyezimungu awape moyo wa subira, familia, jamaa, marafiki na wananchi wa Ludewa, katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao. BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE. -Edward Ngoyai Lowassa

Rais KIKWETE atoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu Deo Filikunjombe na wenzake wawili waliofariki katika ajali ya helikopta

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgombea Urais wa tiketi ya CCM Dkt.John Pimbe Magufuli wakitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa(CCM) Marehemu Deo Filikunjombe na wenzake wawili waliofariki katika ajali ya helikopta juzi katika pori la akiba la mbuga ya Selous. Marehemu aliagwa katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mke wa Marehemu Bi Sarah Filikunjombe wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015. (picha na Freddy Maro)

SIRI YAFICHUKA YA CHANZO CHA AJALI YA CHOPA ILIYO MUUA "DEO FILIKUNJOMBE"

Image
Dar es Salaam. Mgombea ubunge wa Jimbo la Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe na wenzake watatu, akiwamo Kepteni William Silaa wamefariki dunia katika ajali ya helikopta, ambazo wataalamu wanasema husababishwa na kosa la kibinadamu la rubani. Katibu wa Bunge, Thomas Kashilillah alisema jana kuwa walipata taarifa ya ajali hiyo na kuthibitisha kuwa watu wote wanne waliokuwa kwenye helikopta hiyo walifariki dunia. Miili ya Marehemu Filikunjombe, Kepteni Silaa na wengine iliwasili jijini Dar es Salaam jana jioni kwa helikopta ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, lakini hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu taratibu za mazishi. Hii ni ajali ya sita ya ndege aina ya helikopta, maarufu kwa jina la chopa, katika kipindi cha miaka miwili huku Filikunjombe, ambaye alikuwa mbunge wa Ludewa kuanzia mwaka 2010, akiwa mgombea wa tano kupoteza maisha tangu mchakato wa Uchaguzi Mkuu uanze. Mbali na ajali iliyomuhusisha Joshua Nasari mkoani Arusha, nyingine ilitokea Aprili mwaka jana ikimuhusisha mgo

DK. MAGUFULI AONGOZA KUAGA MWILI WA DEO FILIKUNJOMBE

Image
  Dr Magufuli akiwa lugalo hospital kumuaga marehemu Deo Filikunjombe.halo akiwa na mke wa marehemu.

ERIC SHIGONGO: NENDA KAMANDA WANGU DEO

Image
Nakupenda Deo Nimesikitishwa sana na kifo chako. Kweli kifo kipo na kila mmoja wetu atakipitia lakini cha aina hii, cha kijana aliyekuwa akipigania watu wake kiasi hiki? Kinaumiza sana, hata hivyo, hatuna budi zaidi ya kukubali kuwa Deo Filikunjombe, jembe la mkono limeondoka. Chopa iliyosababsha kifo cha Filikunjombe, Capt. William Silaa na watu wengine wawili. Nasema kutoka ndani ya moyo wangu, taifa limepoteza mtu muhimu sana, hakusita kupigania alichokiamini bila uoga wala hofu! Wakati mwingine alitofautiana na msimamo wa chama chake kwa maslahi ya Watanzania maskini, kwako ukweli ulikuwa nguzo. Nenda Deo, nenda kapumzike muda si mrefu tutaungana nawe, kila mwanadamu atafariki dunia maana ndivyo ilivyoandikwa. Lakini cha muhimu ni mtu atakuwa anafanya nini wakati anakufa! Je, atakuwa akiiba au akifanya uzinzi? Deo umekufa ukitumikia watu wako, umekufa kifo chema na Wanaludewa watakuombea. Nenda Deo, pumzika Deo, mema yako yamekutangulia. Hayo ndyo yatakutetea mbele ya

MIILI YA MAREHEMU DEO FILIKUNJOMBE NA WENGINE WAWILI YAAGWA LUGALO

Image
Mbunge wa Jimbo la Ludewa aliyekuwa anamaliza muda wake, Deogratias Filikunjombe enzi za uhai wake. Majeneza yenye miili ya marehemu yakiandaliwa kwa kuagwa. Ndugu, jamaa na marafiki wakipita kwenye majeneza yenye miili ya marehemu kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho. Waombolezaji wakionekana wenye huzuni wakati wa kuaga miili ya marehemu.… Mbunge wa Jimbo la Ludewa aliyekuwa anamaliza muda wake, Deogratias Filikunjombe enzi za uhai wake. Majeneza yenye miili ya marehemu yakiandaliwa kwa kuagwa. Ndugu, jamaa na marafiki wakipita kwenye majeneza yenye miili ya marehemu kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho. Waombolezaji wakionekana wenye huzuni wakati wa kuaga miili ya marehemu. Zoezi la kuaga miili ya marehemu hao likiendelea. Waombolezaji wakiwa katika msitari kuelekea eneo yalipowekwa majeneza hayo kwa ajili ya kuaga. Mke wa marehemu Deo Filikunjombe, Sarah Filikunjombe (kushoto) akilia kwa uchungu. Nyumbani kwa Deo Filikunjombe, Mtoni-Kijichi, Dar es Salaam. P

BARAZA KUU LA WAISLAMU MKOA WA MWANZA LAMUONYA ASKOFU GWAJIMA.

Image
Jana Ijumaa ya Octoba 16,2015 Baraza Kuu la Waislamu Mkoa wa Mwanza liliungana na Waislamu wengine kuadhimisha mwaka mpya wa Kiislamu ambao ni 1437. Kwa kalenda ya Kiislamu sherehe hizo zilifanyika jana tarehe mbili, mwezi Muharamu mwaka wa 1437 (02.01.1437) ikiwa maadhimisho yanayoambatana na kumbukumbu ya Kuhama kwa Mtume Muhammad kutoka Mji wa Macca kwenda Madina. Na: George Binagi-GB Pazzo Katika kuadhimisha sherehe hizo, Baraza hilo kupitia kwa Katibu wake Mkoani  Mwanza Sheikh Mohamed Balla (Kulia Pichani) alitoa tamko kwa niaba ya Waislamu wote Mkoani Mwanza kutokana na kauli inayoelezwa kutolewa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima kwamba ana ndoto ya Misikiti yote nchini kugezwa kuwa Sunday School na Masheikh watakwenda kuangukia katika misalaba. Alisema kauli za namna hiyo si njema kwa mstakabali wa Taifa ambapo alisema kuwa Waislamu wote Mkoani Mwanza wanalaani na kukemea kauli hiyo na nyingine zote za aina hiyo na wale wanaozitoa. Aliwataka Watanzania

RATIBA YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU MH DEO NFILIKUNJOMBE LEO

Image

PICHA ZA AJALI YA CHOPA YA DEO FILIKUNJOMBE

Image
PICHA KWA HISANI YA FRANCIS GODWIN Julius Kambarage Nyerere (13 April 1922 – 14 October 1999)