Wolper Anapozomeana na Kivuli Chake
Jacqueline Wolper Massawe, aliye pia na a.k.a nyingi zikiwemo za Gambe na Amber Rose wa Bongo. MIONGONI mwa waigizaji wa kike niliowahi kufanya naye kazi kwa kipindi kirefu na kwa ukaribu zaidi ni pamoja na mrembo Jacqueline Wolper Massawe, aliye pia na a.k.a nyingi zikiwemo za Gambe na Amber Rose wa Bongo. Mkononi nimefumbata miaka saba sawa tangu nianze kazi ya uandishi wa habari, kwenye magazeti haya pendwa. Ninao uzoefu mkubwa kwa kuwafahamu watu wengi maarufu kwa maana ya maisha yao ndani na nje ya kazi zao, nawajua sana hususan wasanii wa filamu ambao nafanya nao kazi mara kwa mara. Hata wengi wao wananijua vyema , kwenye eneo la kazi kwamba huwa siruki sentensi kwenye kuanika ukweli. Hivi karibuni, Wolper alikaririwa na mmoja wa waandishi wenzangu akisema kitendo cha kumshika na kumbeba mtoto wa mwigizaji mwenzake, Faiza Ally kimemuondolea gundu ya kutopata mtoto hivyo na yeye kutarajia kupata wa kwake mwakani. Sawa, Wolper yuko sahihi lakini mbo...