Posts

Showing posts from August 20, 2015

MAGUFULI ASAINI HATI YA KIAPO YA KUGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA KUU JIJINI DAR

Image
Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi, Dk. John Magufuli  akikabidhi hati ya Kiapo mapema leo mchana kwa Jaji wa Mahakama Kuu, Jaji Sekieti Kihiyo (katikati). Hati ambayo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini katika mahakama kuu jijini Dar es Salaam  Kushoto ni Mgombea Mwenza, Samia Suluhu Hassan.  Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi, Dk. John Magufuli akisaini hati ya Kiapo mapema leo mchana Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.Hati ambayo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini katika mahakamani hapo jijini Dar es Salaam.  Kushoto ni Mgombea Mwenza, Samia Suluhu Hassan.  Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi, Dk. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Jaji Sekieti Kihiyo mara baada ya  kusaini hati ya kiapo mapema leo mchana Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.Hati ambayo kila mgombea wa nafasi ya urais anatakiwa kusaini katika mahakamani hapo jijini Dar es Salaam. Ku...

KIPINDUPINDU CHAENDELEA KUTESA JIJINI DAR ES SALAAM

Image
 Muuguzi Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Nusura Kessy (kushoto), akiwaelekeza wauguzi wa saidizi wake namna ya kuchanganya dawa maalumu ya kuondoa vijiji vinavyoweza kuwa vya ugonjwa wa kipindupindu katika kambi ya wagonjwa walioathiriwa na ugonjwa huo iliyopo Zahanati ya Mburahati Dar es Salaam leo asubuhi. Katika kambi hiyo kuna wagonjwa 21 kati yao watoto ni 7.  Vyombo vikiwekwa kwenye dawa.  Muuguzi Msaidi wa Zahanati ya Mburahati, Maimuna Pazi (kushoto) na Mlinzi wa Zahanati hiyo, Abdallah Mbagala wakisaidiana kuweka dawa maalumu ya kuzuia kuenea kwa vijidudu vya maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu katika vyombo walivyoletewa chakula na ndugu zao katika kambi ya matibabu kwa wagonjwa walioathiriwa na ugonjwa huo iliyopo katika Zahanati ya Mburahati Dar es Salaam leo asubuhi. Dawa hiyo maalumu ikiwekwa katika vyombo vya kutumia. Na Dotto Mwaibale HALI ya ugonjwa wa kipindupindu ulioikumba maeneo kadhaa ya jiji bado inaonesha ni tet...