Posts

Showing posts from July 8, 2017

Malinzi ajiuzulu Urais TFF Akiwa Rumande

Image
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amejiuzulu wadhifa wake wa Ujumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA). Kupitia kwa wakili wake, kampuni ya Rwegoshora, Malinzi amewaandikia barua FIFA kuwataarifu kujitoa kwenye Kamati hiyo kutokana na kuwa mikononi mwa dola kwa sasa. Malinzi, pamoja na Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa na Mhasibu, Nsiande Isawafo Mwanga. wapo rumande hadi Julai 17, upepelezi wa kesi yao utakapokamilika baada ya kunyimwa dhamana Julai 3 katika kesi inayowakabili. Watatu hao walipandishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa mara ya kwanza Juni 29 na kusomewa mashitaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF iliyopo katika banki ya Stanbic, Dar es Salaam. Katika mashitaka hayo, 25 yanakwenda moja kwa moja kwa Rais wa shirikisho hilo, Malinzi akidaiwa kughushi michakato mbalimbali ya kifedha, huku matatu yakiwahusu wote na Katibu wake na Mhasibu wake Nsiande Isaw...
Image
Katika hatua isiyo ya kawaida, binti yake Bwana Trump, Ivanka, alikaa kwa niaba ya baba yake wakati wa kikao kinachohusu Afrika kwenye mkutano wa nchi tajiri wa G20. Vikao vya asubuhi vililenga masuala muhimu ya uhamiaji na afya. Picha iliyowekwa twitter na mmoja wa wapatanishi kutoka Urusi ilimwonyesha Ivanka Trump akikaa katikati ya Rais wa China Xi Jinping na waziri mkuu wa Uingereza, Bi Teresa May. Mwandishi wa BBC katika mkutano huo anasema hakumbuki kuwepo na mipango kama hiyo hapo zamani na kiongozi wa nyadhifa ya juu kama vile waziri wa mambo ya nje, ndio aghlabu huchukua nafasi ya Rais. Bi Trump hakuonekana akishiriki katika mchango wowote kuhusu uhamiaji wa raia wa Afrika kuelekea Ulaya na afya wakati babake alipokuwa ameondoka. Picha ya uwepo wake ilichapishwa katika mtandao wa Twitter na mshiriki mmoja wa Urusi na kuzua hisia kali katia mitandao ya kijamii. Baadhi ya watumiaji wa mitandao hiyo walisema kuwa bi Trump hajachaguliwa wala...

PROFESA JAY AFUNGA NDOA KANISA LA ST. JOSEPH -DAR

Image

Abdi Banda ameaga rasmi Simba

Image
BEKI wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Hassan Banda amefikia makubaliano na klabu ya Baroka F.C ya Afrika Kusini kusaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga nayo. Baada ya kung’ara katika michuano ya Kombe la COSAFA Castle nchini Afrika Kusini akiiwezesha Tanzania kushika nafasi ya tatu, mchezaji huyo wa Simba ya nyumbani, Tanzania sasa anakaribia kwenda kuanza maisha mapya timu hiyo ya Ga-Mphahlele, karibu na Polokwane, Limpopo ambayo inacheza Ligi Kuu ya nchini humo. Banda amesema anaondoka Simba SC aliyoichezea kwa miaka miwili, baada ya kumaliza mkataba wake na hakuwahi kusaini mkataba mpya, hivyo anajiunga na Baroka kama mchezani huru. “Nipo njiani narudi nyumbani kwa ajili ya kuja kuchukua vitu na kurudi rasmi Afrika Kusini kuanza maisha mapya na klabu yangu mpya ya Baroka,”amesema Banda akizungumza kwa simu leo. Banda alikuwemo kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichocheza michuano ya COSAFA Castle na kutwaa Medali ya Shaba baada ya ushindi wa penalti...