Posts
Showing posts from September 19, 2013
AISHA BUI AFUNGUKA JUU YA SHUTUMA ZA KUWA KAFUNGWA UKO BRAZIL
- Get link
- X
- Other Apps
HUKU kukiwa na madai kuwa msanii wa filamu Bongo, Aisha Bui amekamatwa na kufungwa nchini Brazil kwa kunaswa na unga, mwanadada huyo ameibuka na kufafanua juu ya tuhuma hizo. Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita kwa njia ya simu kutokea Brazil, Aisha alisema ameshangazwa na madai hayo wakati yeye yuko nchini humo akiwa amemfuata mchumba wake ambaye jina lake hakuwa tayari kulianika. “Jamani hayo madai ya kwamba nimefungwa huku kwa kesi ya madawa ya kulevya mimi mwenyewe nayashangaa. Niko huku kwa mwezi wa nne sasa, nimekuja kwa mchumba wangu. Hizo taarifa za kwamba eti nimefungwa ni uzushi unaotengenezwa kwa nia ya kunichafua tu. “Wakati naondoka Tanzania ilikuwa kimyakimya kwa kuwa nilijua kuna baadhi ya watu watazusha mambo ya kunipaka matope na ndicho walichokifanya. “Naomba Watanzania wajue niko huru kabisa, naendelea na shughuli zangu kama kawaida. Natarajia kurudi Bongo hivi karibuni,” alisema Aisha .
Rais Jakaya Kikwete atembelea Ubalozi wa Tanzania, Washington, DC
- Get link
- X
- Other Apps
Rais Dkt Jakaya Kikwete akitembea kwa miguu kutoka hotelini kwake kuja kwenye Ubalozi wa Tanzania Marekani siku ya Jumatano Sept 18, 2013 na kukutana na Mabaozi wa Heshima ambao jana Jumatano wasaini mikataba ya kuwa rasmi Mabalozi wa heshima wataofanyakazi wakiiitangaza Tanzania nchini Marekani kwa ajili ya uwekezaji, Utalii na mambo mengine yatakayosaidia kuinua uchumi wa Tanzania. Rais Dkat Jakaya Kikwete akisalimiana na Maafisa Ubalozi wakiwemo wafanyakazi mara tu alipoingia Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo barabra ya 22, Washington, DC Rais Dkt Jakaya Kikwete akitia saidi kitabu cha wageni Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni huku Mhe. Waziri Bernard Membe na Mhe. Balozi Liberata Mulamula wakishuhudia. Raus Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mama William alipokua akiingia chumba cha mikutano cha Nyerere Rais Dkt Jakaya Kikwete...
HIVI NDIO OMMY DIMPOZ ALIVYOWASILI JIJI LA MARAHA, WASHINGTON DC
- Get link
- X
- Other Apps
ASEMA YUPOTAYARI KUACHA HISTORIA MAREKANI KUANZIA JUMAMOSI HII WASHINGTON DC ! OMMY DIMPOZ ALIPOWASILI WASHINGTON DC “OMMY DIMPOZ” AKIWA NA PROMOTER WAKE “DMK GLOBAL” DIMPOZ AKIPATA UKODAKI NA PROMOTER WAKE “MR DMK” PAMOJA NA AKINA DADA WALIOKUWEPO KUMPOKEA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA WASHINGTON DC.KULIA NI MLIMBWENDE ALIYEWAHI KUTWAA TAJI LA MISS TEMEKE NA KUSHOTO NI MLIMBWENDE MWINGINE KUTOKA TZ. OMMY NDANI YA LIMO KUELEKEA HILTON. LUNCH TIME AT THE HILTON. OMMY DIMPOZ AKIWA NA DESIGNER MISS TEMEKE NA GAUNI LAKE LA KWETU FASHION.
Messi amjibu Ronaldo, apiga hat trick, barca ikiua ajax 4-0
- Get link
- X
- Other Apps
Wachezaji wa Baraca wakishangilia pointi tatu Lionel Messi akifunga bao Lionel Messiamejibu mapigo ya mpinzani wake, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid baada ya kuifungia hat-trick Barcelona katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Ajax katika mchezo wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya, Uwanja wa Nou Camp. Muargentina huyo pamoja na kufunga mabao matatu peke yake usiku, pia alitengeneza bao la nne lililofungwa na Gerard Pique. Haikuwa bahati yao, Ajax kwani walikosa hadi penalti baada ya kipa Victor Valdes kuokoa mkwaju wa Kolbeinn Sigthorsson. Messi alifunga mabao yake katika dakika za 22, 55 na 75, wakati Pique alifunga dakika ya 69. Kikosi cha Barcelona kilikuwa: Valdes, Alves, Pique/Bartra dk80, Mascherano, Adriano, Busquets, Fabregas/Xavi dk72, Iniesta, Sanchez, Messi, Neymar /Pedro dk72....
UNAFIKIRI VAZI HILI LINAFAA KUVALIWA WAPI NA WAKATI GANI?
- Get link
- X
- Other Apps
JOHARI AKIRI KUZICHAPA NA HANSI CHUU KISA PENZI LA RAY...HUU NDIO MKANDA MZIMA WATUKIO HILO
- Get link
- X
- Other Apps
Waigizaji wenye majina makubwa Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ na Chuchu Hans wanadaiwa kuchapana kisa kikidaiwa kuwa ni penzi la mwigizaji ‘kaka mkubwa’, Vincent Kigosi ‘Ray’, TUHUMA Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho ni rafiki wa karibu wa wasanii hao, tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ofisi za RJ Productions, zinazomilikiwa kwa ubia wa Ray na Johari zilizopo Sinza-Mori jijini Dar ambapo Johari alikuwa akimtuhumu Chuchu mambo mazito ya kimapenzi kwa Ray. Shushushu huyo alitonya kuwa, siku ya tukio Johari na wasanii wenzake walikuwa wakirekodi filamu ndani ya hoteli moja (jina tunalo) iliyopo jirani na ofisi hizo ndipo alipofikishiwa umbeya kuwa Chuchu yuko kwenye ofisi hizo ‘akijiachia’ na bosi mwenzake (Ray), jambo lililotia ganzi moyoni mwa mdada huyo. MCHEZO MZIMA ‘Kikulacho’ huyo aliendelea kudai kuwa baada ya Johari kupata habari hizo, bila kujiuliza wala kuvuta subira, ‘alisaga soli’ hadi maeneo hayo. “Al...
SHAHIDI AFARIKI GHAFLA MAHAKAMANI WAKATI AKITOA USHAHIDI HUKO MKOANI MARA...!!
- Get link
- X
- Other Apps
Katika hali isiyo ya kawaida, mkazi wa Kijiji cha Lorwe Kata ya Nyahongo Shirati, wilayani Rorya, mkoani Mara, Charles Warito (38), ambaye ni shahidi wa mlalamikaji katika Kesi ya kudhuru mwili kwa kujeruhiwa vibaya kwa kukatwa mkono na kusababisha ulemavu amefariki dunia, wakati akitoa ushahidi. Warito alikutwa na umauti huo akiwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime mbele ya Jaji G. Ndika anayesikiliza kesi katika Wilaya za Tarime na Rorya. Tukio hilo la kusikitisha lilitokea jana mchana baada ya Mwanasheria wa Serikali, Mayega na Mwendesha Mashitaka wa Polisi Inspekta George Lutonja walimwita kuingia Kizimbani tayari kutoa ushahidi. Shahidi huyo alianza kutoa ushahidi wake na alieleza kushambuliwa kwa kukatwa mapanga na mtuhumiwa Kichohe Kichere ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Omoche Kata hiyo ya Nyahongo Shirati Januari 26, mwaka 2008 na kutokana na majeraha aliyoyapata kwa kukatwa mkono na mwili wake ulianza ku...
RIPOTI YA GAZETI LA RAIA MWEMA KUHUSU KUACHIWA HURU KWA AGNESS MASOGANGE NA MELLISA
- Get link
- X
- Other Apps
WATANZANIA wawili, Agnes Gerald (Masogange) na mwenzake Melissa Edward waliokamatwa nchini Afrika Kusini kwa madai ya kusafirisha kilo 150 za dawa za kulevya wanayo nafasi kubwa ya kuachiwa wakati wowote kuanzia sasa, Raia Mwema limeambiwa. Ingawa ripoti za awali zilieleza kwamba Watanzania hao walikuwa wamesafirisha kilo 150 za dawa aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania, imebainika kwamba adawa walizobeba zinafahamika kwa jina la Ephedrine ambazo hazimo katika kundi la dawa za kulevya. Watanzania hao walikamatwa nchini Afrika Kusini katika Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo jijini Johannesburg wakiwa na dawa hizo zilizokadiriwa kuwa na thamani ya Sh bilioni 6.8. Hata hivyo, Ephedrine –dawa ambayo sasa imebainika kuwa ndiyo waliyosafirisha akina dada hao inaangukia katika kundi la vibashirifu (precursors) yaani dawa ambazo malighafi yake inaweza kutumika...