Posts

Showing posts from May 11, 2016

TAZAMA PICHA ZA MTOTO WA VAN DAMME AKIFANYA MAMBO ALIYOKUWA AKIFANYA BABA YAKE

Image
Bianca, binti wa Van Damme Mtoto wa nyoka naye ni nyoka vile vile.  Uzuri wa Bianca Van Varenberg, 25, usikulaghai ukadhani ni binti wa kuchezea tu. Atakupa mkong’oto hadi usahau njia uliyopitia.  Ni mtoto wa muigizaji mkongwe wa movie za mapigano, Jean Claude Van Damme. Anajulikana zaidi kikazi kama Bianca Bree. Miaka mitano iliyopita alionekana kwenye uzinduzi wa filamu ya baba yake lakini akawa kimya tena, hadi sasa. Mwaka 2012 alisema angependa atoke kinyake bila kutumia jina la baba yake ndio maana hajaliweka kwenye majina yake. Yeye pia anapenda kuja kuwa muigizaji wa filamu.

SNURA :CHURA IMENIONGEZEA UMAARUFU

Image
STAA wa Muziki wa Kizazi Kipya, Snura Mushi amefunguka kuwa licha ya changamoto ya kutakiwa kutengeneza video mpya yenye maadili ya wimbo wake wa Chura, umaarufu wake umeongezeka kwani jina lake limekuwa gumzo kila kona nje na ndani ya nchi.  Akipiga stori na gazeti hili, Snura alisema tangu aanze muziki hajawahi kufanya mahojiano na watu wengi kama kipindi hiki, kwani japokuwa alitakiwa na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kurekebisha wimbo huo, amepata faida kubwa kimuziki na kiakili. “Ukiachana na changamoto nimefarijika sana kwani jina langu limekuwa gumzo kila kona, nimepata elimu ambayo sikuwa nayo ambapo wizara imenipa ubalozi wa kuwafundisha wenzangu wasitoe nyimbo zisizokuwa na maadili, hivyo kila ninapokutana na wasanii wenzangu nawafundisha,” alisema

GADNER SIJUTIA KUMTUSI KOMANDO JIDE,MAMBO MAZITO YAIBUKA

Image
SIKU chache baada ya kipande cha video kuonekana katika mitandao ya kijamii, ikimuonesha mtangazaji maarufu, Gardner G Habash akitoa maneno ya matusi kwa mkewe wa zamani, Judith Wambura ‘Jide’, ameonekana kujutia kitendo chake hicho. Katika eneo ambalo linalotajwa kuwa ni katika Ukumbi wa TCC Chang’ombe, Ijumaa ya wiki iliyopita, Gardner, aliyejitambulisha kuwa ni Mtangazaji wa Clouds FM, alitoa maneno ya kidhalilishaji kwa msanii huyo wa Muziki wa Kizazi Kipya, baada ya kuulizwa na mashabiki kama alikuwa na matatizo na mtalaka wake. “Mimi sina neno na yule mtoto wa kike, nime… (tusi) kwa miaka 15,” alisema mtangazaji huyo, ambaye aliishi katika maisha ya ndoa na Jide kwa zaidi ya miaka kumi, kabla ya kutengana miaka miwili iliyopita Akizungumza na Risasi Mchanganyiko lililotaka kufahamu kisa na mkasa wa kutoa maneno hayo, Gardner alishindwa kuongea akidai alikuwa katika kikao, lakini alituma ujumbe mfupi wa maneno akisema;  Gardner, aliye...

Chadema Kuijadili Serikali ya Rais Magufuli

Image
Kamati Kuu ya Chadema itakutana mjini Dodoma katika kikao chake cha kikatiba kuanzia Mei 11 Jumatano na Alhamisi kitakachojadili mwenendo wa Serikali ya CCM chini ya Rais John Magufuli. Taarifa iliyotolewa leo na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Tumaini Makene imesema kikao hicho, pamoja na mambo mengine, kitajadili taarifa ya hali ya siasa nchini. Pia kikao hicho kitajadili na kupitisha mpango kazi wa chama kwa mwaka huu unatokana na Mpango Mkakati wa Chama wa miaka 5 kabla ya Sekretarieti kuanza utekelezaji. Mpango huo utahusisha shughuli mbalimbali za chama ikiwa ni pamoja na uimarishaji wa chama nchi nzima na kuendelea kuwatumikia wananchi