Rais JPM Awaongoza Mamia Kuagwa Mwili wa Samuel Sitta Karimjee Dar
Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akiongoza waombolezaji kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Spika wa Bunge Mstaafu, Samuel John Sitta. …Akiwapa mkono wa pole wafiwa wa marehemu Sitta baada ya kutoa heshima za mwisho mbele ya jeneza. Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete akipita mbele ya jeneza kutoa heshima zake za mwisho. Makamu wa Rais Mstaafu, Dk. Gharib Bilal akipita mbele ya jeneza kuuaga mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge Mstaafu, Samwel Sitta. Viongozi mbalimbali wakiwa msibani hapo. Mbunge wa Muleba Kusini, Prof. Anna Tibaijuka (katikati) akiwa na waombolezaji wengine katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. …Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi naye akipita mbele kuuaga mwili wa marehemu Sitta. Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye akipita mbele ya jeneza kuuaga mwili wa marehemu. Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba naye akipita mbele ya jeneza kutoa heshima za mwisho. ...