MKE WA TU AFUMWA LIVE NA MCHEPUKO GESTI WAKIFANYA YAO JIJINI DAR
Issa Mnally na Richard Bukos AMA KWELI duniani kuna mambo! Wakati wakazi wengi wa Jiji la Dar es Salaam wakiwa katika harakati za kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, dada mmoja ambaye ni mke wa mtu yeye alijikuta akiiserebukia kwa fumanizi gesti, tena akiwa na mume wa mtu! Tukio hilo lilijiri Alhamisi Kuu maeneo Buza jijini Dar, mishale ya saa 7:00 usiku huku jamii ikiwa katika harakati za kununua hiki na kile kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka iliyoadhimishwa duniani kote jana huku leo ikiwa ni Jumatatu ya Pasaka. Katika fumanizi hilo, timbwili la aina yake liliibuka baada ya mwanamke huyo mwenye mwili mkubwa, kuponyoka mikononi mwa mke aliyemnasa na kutoka nduki nje akiwa mtupu bila kujali hali hiyo. MADAI YA AWALI Awali, ilidaiwa kuwa mume huyo wa mtu aliyefahamika kwa jina la baba Somoe, mkazi wa Kongowe (nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam) alimchepuka mke wake (mama Somoe) na kuanzisha uhusiano na mwanamke huyo. MKE ATILIA SHAKA, AFUATILIA Chanzo kikazidi kudai kwa...