Posts

Showing posts from June 26, 2016

Black Coffee Ashinda Tuzo ya BET ya Best International Act Africa

Image
Black Coffee baada ya kupokea tuzo yake. Black Coffee akiwa na mkewe Enhle Mbali Mlotshwa. Black Coffee na mkewe wakiwa kwenye pozi na baadhi ya mastaa kutoka Afrika akiwemo Akon na AKA.   Black Coffee katika pozi. Black Coffee amekuwa mwanamuziki wa kwanza kutoka Afrika Kusini kutwaa tuzo ya BET katika kipengere cha ‘Best International Act Africa 2016’ na kuwapiku mastaa wengine walioteuliwa kuwania tuzo hiyo akiwemo Diamond Platnumz. Black Coffee mwenye umri wa miaka 40, ametwaa tuzo hiyo huko Los Angeles nchini Marekani akiwabwaga wasanii wenzake ambao ni AKA‚ Cassper Nyovest‚ Diamond Platnumz‚ MzVee‚ Serge Beynaud‚ Wizkid na Yemi Alade waliokuwa wanawania tuzo hiyo.

Rais Magufuli Afanya Mabadiliko ya Ma RC na Ma DC

Image
Rais Dk. John Pombe Magufuli. Rais Dk. Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya, atengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo na kuteua Ma DC 139. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya mabadiliko madogo katika safu ya wakuu wa mikoa na amewateua wakuu wa wilaya 139. Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R. Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Bi. Zainab R. Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa. Rais Magufuli pia amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma. Dkt. Binilith Satano Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam am...

Meli ya Mizigo Yazama Unguja

Image
Zoezi la uokoaji likiendelea eneo ilipozama meli ya MV Happy. Meli ya mizigo iitwayo MV Happy iliyokuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kwenda Zanzibar imezama leo asubuhi kwenye Bahari ya Hindi eneo la Chumbe, Unguja. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo ni kwamba meli hiyo ilianza kuzama majira ya saa 10 alfajiri na kufikia saa moja asubuhi ilikuwa imezama kabisa ndani ya maji. Wananchi wakishuhudia zoezi la uokoaji. Mpaka sasa hakuna vifo vilivyoripotiwa bali mizigo iliyokuwemo kwenye meli hiyo ndiyo iliyozama. Taarifa zaidi zitaendelea kuwajia kupitia tovuti hii.

Tanzia: Aliyekuwa Mbunge wa Biharamulo Magharibi (2010-2015) Afariki

Image
Dk. Antony Gervase Mbassa enzi za uhai wake. Aliyekuwa Mbunge wa Biharamulo Magharibi (2010-2015) kupitia CHADEMA, Dk. Antony Gervase Mbassa amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake.

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA MPANGO WA KITAIFA WA KITUO CHA MAWASILIANO CHA JESHI LA POLISI (CALL CENTRE)

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua kituo cha mawasiliano ya polisi (Call centre) katika kituo cha Kati jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi. .Pamoja naye ni Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Ndani Meja Jenerali Projest  Rwegasira, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine  wa sekta ya umma na binfasi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  akikagua kituo cha mawasiliano ya polisi (Call centre) katika kituo cha Kati jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi. .Pamoja naye ni Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Ndani Meja Jenerali Projest  Rwegasira, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine  wa sekta ya...