Posts

Showing posts from November 11, 2017

BASATA yaongea kuhusu Msondo Ngoma kumdai Diamond Milioni 300

Image
Baada ya Band ya Msondo Ngoma kutaka ilipwe shilingi milioni 300 na kundi la WCB kwa kutumia bila ruhusa vionjo vya wimbo wake kwenye wimbo wa “Zilipendwa”  Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mngereza ameongea yafuatayo. “Unaweza kuitazama katika mitizamo mbalimbali lakini unapoangalia kwamba wanaanza kushtakiana kimsingi ni taratibu ambayo inagusa sana mambo ya haki miliki, kabla ya kuitumia kazi ya mtu ni vizuri ukamuona mwenye kazi mkubaliane” “Ukitumia kazi ya mtu bila utaratibu hiyo moja kwa moja ni kosa, cha msingi hata kabla ya kumuweka Mwanasheria ili kudai haki yako ni vizuri ukawafata au ukawasiliana na alietumia kazi yako bila ruhusa…. katika hili linalojitokeza sasa hivi ni swala la kuamshana kwamba kazi ya sanaa ya mtu flani haina tofauti na mali ya mtu ya aina nyingine, huwezi kutumia gari la mtu bila ridhaa yake” – Mngereza

Ajali yaua na kujeruhi Moshi

Image
Watu kadhaa wanasadikika kufariki na wengine kujeruhiwa kwenye ajali ya gari iliyotokea mchana huu mkoani Kilimanjaro ikihusisha roli na gari ndogo aina ya Noah ya abiria ya Sanya Juu - Moshi Ajali hiyo mbaya imetokea mchana  huu maeneo ya Kikavu  karibu na Kwasadala Mkoani Kilimanjaro ambapo Roli kubwa lilikuwa linajaribu kulipita gari lingine  ndipo likakutana uso kwa uso  na Gari ndogo aina ya Noah iliyokuwa imebeba abiria likitokea Moshi mjini kwenda  Sanya Juu. Taarifa kamili za ajali hiyo bado hazijatolewa lakini mashuhuda wa tukio wanasema huenda baadhi ya abiria waliokuwa kwenye Noah wamejeruhiwa. Aidha mashuhuda hao wameeleza kuwa watu wanne ndio wanaonekana kuwa bado ni majeruhi lakini hali zao ni mbaya na taratibu za kuwafikisha hospitali kwaajili ya matibabu zinaendelea. Hata hivyo bado majina ya abiria waliokuwemo kwenye Noah hayajapatikana mara moja tunaendelea kufuatilia taarifa kamili kutoka kwa kamanda wa Polisi mk...

AJALI; Wawili wafariki katika ajali wilayani Ikungi

Image
Watu wawili wamekufa papo hapo na wengine wawili wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Ikungi,kufuatia gari aina ya Toyota Landcruiser kugongana uso kwa uso na basi la Taqwa.                                                                                            Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Sigida SSP Isaya Mbughi amesema,ajali imetokea katika kijiji cha Kideka wilayani Ikungi  majira ya saa tano asubuhi na imehusisha basi la Taqwa lenye usajili wa nambat 159 CWH lilokuwa likitokea Kampala  nchini Uganda na kuelekea jiji Dar-es-Salaam ,kugongana uso kwa uso na gari ndogo aina ya Toyota Landcruiser yenye usajili wa namba T 862 DJN ilyokuwa ikitokea Dodoma,na kusema chanzo cha ajali ni ...

Wema Sepetu apata pigo hili

Image
  Serikali kupitia mamlaka zake imezifungia rangi za midomo zinazozalishwa na Mwanadada aliyewahi kuwa Miss Tanzania na Muigizaji wa Filamu, Wema Sepetu. Rangi hizo zinajulikana kwa jina la "Kiss". Kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) pamoja na Shirika la Viwango Nchini(TBS) wamebaini kuwa rangi hizo hazina ubora kwa matumizi ya binadamu. Kwa upande wa Meneja wa Wema Sepetu, Happy Shame alipotakiwa kuzungumzia suala hilo amefunguka na kusema kwamba taarifa za kufungiwa kwa bidhaa hizo yeye kama Meneja hajazipata bali anachofahamu mzigo ulikuwa haujaingia sokoni na kwamba muigizajin huyo alikuwa bado akifuatilia vibali kutoka mamlaka husika. Rangi hizo za mdomo za muigizaji Wema Sepetu zilizinduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015 usiku wa birthday yake.

Watanzania 200 kupata ajira Saudi Arabia

Image
Kampuni ya Bravo Job Centre Agency Limited ya malkia wa urembo nchini Tanzania, Sitti Mtemvu imeweza kutafuta nafasi za ajira 200 kwa Watanzania nchini Saudia Arabia ambapo usahili utafanyika kesho. Sitti amesema hayo leo Uwanja wa ndege wa JK Nyerere wakati akiwapokea wawakilishi wa Kampuni ya Almarai ambayo inaratibu usahili huo.  Alisema usahili huo utafanyika nyuma ya National House Temeke, karibu na Uwanja wa Taifa ambapo usaili huo utafanyika kwa makundi hivyo wataokuwa na sifa watachukuliwa na kwenda kufanya kazi nje ya. Aliongeza kuwa watu wenye fani na sifa za udereva, upishi au daktari wanaombwa wafike kesho ili waweze kupata nafasi za ajira ambazo zitakuwa ni za haki na stahiki zote kama mfanyakazi atakuwa anazipata kupitia mkataba wake .