Kajala amtolea chozi kigogo wa Wema!
Kajala Masanja Na Imelda Mtema Siku chache baada ya gazeti dada na hili, Risasi Jumamosi kuandika juu ya aliyekuwa kigogo wa msanii Wema Sepetu, Clement Kiondo ‘CK’ kunaswa akiuza mishikaki, tukio hilo limemliza shosti wa Wema, Kajala Masanja. Kumwaga chozi kwa Kajala kumetokana na maelezo yake kwamba, baada ya kuiona habari hiyo hakuweza kuamini kama kweli ni CK yule aliyewahi kumtolea shilingi milioni 13 kama faini ili asiende jela kutokana msala aliokuwa nao. Wema Sepetu Akizunbumza na Ijumaa kwa majonzi, Kajala alisema: “Kiukweli nililia sana, nilishindwa kuamini kama kweli CK amefikia hali hiyo,” alisema Kajala ambaye pia aliwahi kudaiwa kutoka kimapenzi na jamaa huyo. Akasema stori hiyo isingekuwa imeambatana na picha asingeamini lakini alipoona zile picha zinazomuonesha CK akiwa jikoni akimhudumia mtu, alishindwa kujizuia na kujikuta akibubujikwa na machozi. Tukio la kunaswa kwa CK akiuza mishikaki lilinaswa na mapaparazi wetu juzikati kwenye baa m...