Posts

Showing posts from August 28, 2015

Maandalizi Ya Uzinduzi Wa Kampeni Za UKAWA Jangwani

Image
"Nimealikwa kuzungumza na wanawake wa jiji la Dar Es Salaam. Nimewaambia kuwa UKAWA tunatambua kuwa wanawake ndio msingi wa taifa letu na tumejipanga vizuri kuzimaliza changamoto zinazowakabili. Kiupekee nampongeza Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA, Mheshimiwa Halima Mdee na Mama Regina Lowassa kwa hotuba zao zenye kuhamasisha ukombozi miongoni mwa wanawake. Nimetumia fursa hiyo pia kutoa shukrani za pekee kwa wanawake wote nchini kwa kuendelea kuniunga mkono. Nimesisitiza pia wajitokeze kwa wingi kutupigia kura ili kwa pamoja tulete mabadiliko na tuanze mapambano ya kumaliza tatizo la umaskini hapa nchini. Tuko Tayari kwa Mabadiliko".- Edward Ngoyai Lowassa

MAGUFULI AZUNGUMZA NA WAJUMBE WA JUMUIYA YA WAZAZI YA CCM

Image
Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akiingia kwenye Ukumbi wa Karemjee kuzungumza na Wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM. Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wajumbe hao. Dkt. Magufuli amewaomba wajumbe hao kufanya kazi kwa uadilifu na kuihubiri Amani ya nchi yetu ili maendeleo bora yaweze kupatikana. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Abdalah Majura akizungumza katika mkutano huo. Wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi Taifa wakimshangilia Mgombea wa CCM-Dkt. John Magufuli.   Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Ushindi Adam Malima. Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe hao.

NJEMBA Yafanyiwa KITU MBAYA Mbele ya Mkewe!

Image
  Akiminyiwa kichapo. Richard Bukos Hii kali! Njemba mmoja ambaye jina halikupatikana amekula kipigo mbele ya mkewe ambaye alifanikiwa kukimbia baada ya kudaiwa kufanya jaribio la kuingia kwenye onesho la Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ kwa kutumia tiketi feki, Ijumaa lina kisa na mkasa. Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Ukumbi wa Club East 24 iliyopo Mikocheni jijini Dar ambapo jamaa huyo alifika kwa Bajaj, akiwa na mrembo matata aliyetinga viatu virefu vya mchongoko na kigauni kifupi. Wawili hao walishuhudiwa wakisogelea getini kwa mikogo huku wakiwa wameshikana viuno ambapo nuksi ilianzia pale walipowafikia wasimamizi wa getini na kuwaonesha tiketi. Katika hali ya kushangaza, ghafla jamaa huyo alishtukia akilambwa kofi la uso na baunsa wa Kampuni ya Black Ninja aliyefahamika kwa jina moja la Hamidu na kuanza kuhojiwa alikoipata tiketi hiyo. Wakati akijiandaa kujibu, yule mwanamke aliyekuwa na...

DK. SLAA KUJIUNGA NA UZINDUZI WA UKAWA JANGWANI”

Image
Wakati ambapo vyama vya upinzani vinatarajia kuzindua kampeni zake katika uwanja wa Jangwani kesho na kumnadi mgombea wake wa urais, Edward Lowassa, duru zinaeleza kuwa huenda Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa akahudhuria uzinduzi huo.Mmoja kati ya viongozi wa Chadema ambaye alinukuliwa na gazeti moja kubwa nchini huku akitaka jina lake lisitajwe, alisema kuwa zipo taarifa za chinichini ndani ya chama hicho zinazoeleza kuwa Dk. Slaa ataibuka Jangwani kesho“Zipo taarifa za chinini kuwa Dk. SSlaa atahudhuria uzinduzi, hatujui zina ukweli kiasi gani na atashiriki kama Katibu Mkuu au mgeni mwalikwa, kama atahudhuria, atatusaidia sana na asipokuja suala lake litaendlea kuwachanganya wafuasi wa Chadema,” alinukuliwa kiongozi huyo wa Chadema.Haijafahamika kama taarifa hizo ni za kweli au la kwa kuwa hata uamuzi wa kumkaribisha Edward Lowassa kujiunga na Chadema ulifanywa kuwa siri kubwa kwa viongozi wachache sana takribani miezi mitatu kabla. Hata viongozi wengine wa...

SOMA MAGAZETI YOTE YA LEO IJUMAA HAPA

Image
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .