Posts

Showing posts from August 25, 2017

Waziri Lukuvi: "Bomoabomoa hainihusu"

Image
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amefunguka na kusema zoezi la bomoabomoa linaloendelea jijini Dar es Salaam katika maeneo ya Kimara na Kibamba yeye halimuhusu hivyo awataka watu wamuulize Waziri wa ujenzi, uchukuzi Waziri Lukuvi alisema zoezi linaloendelea Kimara na Kibamba ni sheria ya barabara ndiyo inayofanya ile kazi na siyo yeye na kuwataka watu wamtafute Waziri husika ili aweze kuwapa maelezo juu ya jambo hilo. "Hapana siwezi kuzungumzia hilo nenda kamuone Waziri wa Ujenzi kwani Sheria ya barabara ndiyo inayofanya ile kazi siyo mimi hivyo siwezi kuzungumza lolote kwenye hilo jambo kwani mimi bomoabomoa hiyo hainihusu, kwani kila mtu anaapa kwa kipande chake na mimi siyo Waziri wa jumla, Waziri wa jumla ni Waziri Mkuu" alisema Lukuvi  Aidha Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimelaani vikali zoezi la bomoabomoa linaloendelea katika maene...

Taarifa muhimu kwa wote walioomba na watakaoomba kazi Serikalini

Image
Mtakumbuka Serikali katika mwaka wa fedha uliomalizika 2016/2017 iliahidi kutoa Ajira serikalini zaidi ya 52,000 kwa Watanzania, ambapo katika siku za hivi karibuni Serikali imekuwa ikitoa vibali vya kuajiriwa watumishi wa kada mbalimbali ikiwemo Waalimu wa Sayansi, Kada za Afya na maeneo mengine kulingana na mahitaji. Kama mnavyofahamu mojawapo ya jukumu la msingi la kuanzishwa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni pamoja na kuendesha mchakato wa ajira kwa niaba ya waajiri mbalimbali na hatimae kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi wanaofaulu usaili, ambapo tangu Serikali ilipoanza kutoa vibali baada ya kusitishwa tumeshapokea jumla ya vibali kwa ajili ya mamlaka za Ajira 239, kati ya hivyo vipo ambavyo vimeshafanyiwa kazi na vingine mchakato wake unaendelea katika hatua mbalimbali. Aidha, baadhi ya vibali ambavyo mchakato wake umeshakamilika ni pamoja na  kibali cha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ambayo tulipokea jumla ya  maombi ya...

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 25.08.2017

Image

MAGAZETI YA UDAKU LEO

Image
  

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

Image

RAIS MAGUFULI ASEMA NIMEAMUA KUPAMBANA NA RUSHA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli amesema kuwa Tanzania ikifanikiwa kuondoa rushwa angalau kwa kwa asilimia 80 nchi itafanikiwa kuondoa matatizo mengi. Rais Magufuli ameyazungumza hayo leo hafla ya kuwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es salaam akiwemo Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU. “Tukifanikiwa kupunguza rushwa angalau kwa asilimia 80 nchi ittafanikiwa kuondoa matatizo mengi, na ni vema mtambue kuwa hatua hizi tunazochukua zimeanza kuwavutia wafadhili wengi na wawekezaji,” “Na mimi kama kiongozi wenu nimeamua kupambana na rushwa kikweli kweli na ninawaomba nyote mshirikiane kuondoa rushwa katika maeneo yenu ya kazi,” amefafanua Rais Magufuli.

RAIS MAGUFULI ATAJA KITU KINACHOMKERA TAKUKURU

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameelezwa kutoridhishwa na taratibu za uchunguzi na uendeshaji wa mashitaka ya rushwa zinavyochukua muda mrefu na ametoa wito kwa viongozi wa TAKUKURU kufanyia kazi eneo hilo ili vita dhidi ya rushwa ionekane ikizaa matunda haraka. Rais Magufuli ameyazungumza hayo leo hafla ya kuwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es salaam akiwemo Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU. Hata hivyo Rais Magufuli ameipongeza TAKUKURU kwa kazi wanayoifanya lakini huku akitaka juhudi ziongezwe zaidi ili watu wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa vya kutoa na kupokea rushwa washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.