OBAMA ASEMA BANGI NI BORA KULIKO POMBE. SOMA ALICHOKISEMA ZAIDI HAPA
President Barack Obama wa Marekani amesema kuvuta bangi ni salama zaidi kuliko kunywa pombe lakini akawasisitizia mabinti zake kwamba hilo sio wazo zuri pia ambapo kwa mujibu wa gazeti la The Mirror, amesema anaamini uvutaji bangi hauna madhara au athari za hatari kwa mtumiaji binafsi. Obama ambae aliwahi kuvuta kwenye enzi za ujana wake anasema “uvutaji sio kitu ambacho nachochea kifanyike, tambua ni upotezaji muda na inaathiri afya, bangi imehalalishwa kwenye miji ya Colorado na Washington kwa kura ya maoni na ilikuwa ni muhimu kwa ajili ya mataifa kumaliza uhalifu wa vijana wadogo wanaotoka kwenye familia zenye asili ya umasikini” “tabaka la watoto wa kati hawafungwi kwa uvutaji bangi bali wanaofungwa ni wale watoto wa maskini, watoto wenye asili ya African -American na wa Kilatino wengi wao hawana uwezo wa kuwa rasilimali au misaada kuweza kuepuka vifungo vikali, hatupaswi kufunga watoto wetu au watumiaji binafsi vifungo virefu vya jela wakati baadhi ...