P FUNK AFUNGA NDOA YA SIRI
BAADA ya kuishi maisha ya kisela kwa muda mrefu, hatimaye mtayarishaji nguli wa muziki Bongo, Paul Mathyasse ‘P Funk’ ameoa kwa siri. Mtayarishaji nguli wa muziki Bongo, Paul Mathyasse ‘P Funk’ wakati wa harusi yake. Taarifa kutoka kwa chanzo makini kilichoshuhudia tukio hilo, lilichukua nafasi jijini Arusha mwishoni mwa wiki iliyopita kwa usiri mkubwa. Imeelezwa kuwa, P Funk aliamua kumuoa rasmi mzazi mwenzake, Samira baada ya kuishi naye kwa miaka kadhaa kama mke na mume lakini haikujulikana mara moja sababu za kuweka usiri katika tukio hilo la kheri. Maharusi wakipongezwa na ndugu na jamaa zao baada ya ndoa. “Jamaa (P Funk) amevuta jiko rasmi kwa siri kubwa lakini ameamua kufanya siri hata sijui ni kwa nini, tukio limechukua nafasi huku Arusha na watu kadhaa walialikwa lakini mastaa siyo wengi. “Sherehe imefana, watu wamekula, wamekunywa kwelikweli maana misosi ilikuwepo ya kumwaga,” kilisema chanzo hicho. Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, ka...