Posts

Showing posts from September 17, 2015

RAIS KIKWETE AZINDUA MAJENGO PACHA YA GHOROFA 35 YA PSPF TOWERS MTAA WA SOKOINE JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Image
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa pensheni wa PSPF Bw.  Adam Mayingu alipowasili kuzindua majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015  Mrisho Mpoto na Mjomba Band wakitumbuiza kwenye sherehe za  majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dr. Ramadhani Dau   alipowasili kuzindua majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015   majengo pacha ya ghorofa 35 ya PSPF TOWERS mtaa wa Sokoine jijini Dar es salaam yaliyozindulia  leo Septemba 16, 2015   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea jambo na  Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa pensheni wa PSPF  Mkurugenzin Mkuu  wa  Mfuko  wa  Pensh...

Wafanyakazi waliofichua ukweli kuhusu kikao cha Dr. Slaa Serena Hotel wafukuzwa kazi

Image
Kama mnavyokumbuka mwezi huu tarehe 1 aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema Dr Slaa aliitisha kikao cha waandishi wa habari pale Serena Hotel, ambapo mkutano huo ulirushwa LIVE na vituo vya televisheni vipatavyo vitano na radio kadhaa nazo zikarusha mkutano huo moja kwa moja. Katika mkutano huo alitangaza rasmi kujivua Ukatibu Mkuu wa Chadema na uanachama pia wa Chama hicho na kueleza kuwa anastaafu kabisa shughuli za siasa na kwa hiyo akaeleza kuwa hana nia ya kujiunga na chama chochote cha siasa. Hata hivyo katika kikao hicho ambapo alitumia zaidi ya saa 1 kuongea ambapo alikitumia kikao hicho karibu chote kuporomosha mashambulizi mfululizo kwa chama chake cha Chadema na vyama vinavyounda Ukawa na kumshambulia Edward Lowassa kwa nguvu zake zote na kumuita fisadi mkubwa na kukilaumu chama chake kwa kumpokea Lowassa na kupewa fursa ya kugombea Urais kwa tiketi ya chama cha Chadema kuwa ni sawasawa na kukihamisha choo kutoka chumbani na kukipeleka sebuleni. Baada ya kika...