Posts

Showing posts from May 23, 2017

COUPLE YAJIUWA, YAACHA UJUMBE MZITO KISHA KUJITUPA MTONI

Image
Mume na mke walioamua kujitupa ndani ya mto kwa kile walichokiita 'mkataba wa kujiua'  wameacha ujumbe na kusema kwamba hiyo imewalazimu baada ya kuona kuwa hakuna msaada kwa ajili ya afya ya akili ya mwanamke. Jennifer Slack, 63, na mume Graham, 62, walikufa maji katika Mto Yare Couple iliacha ujumbe kwa madai Bibi Slack hakupata 'msaada' kwa matatizo ya akili.  Uchunguzi umesema kulikuwa na ucheleweshaji wa kesi yake zinashughulikiwa na shirika la NHS trust. Mstaafu muuguzi Jennifer Slack, 63, na mume wake Graham, 62, wamejifunga wenyewe pamoja na kujitupa kwenye Mto Yare katika eneo maarufu kama Gorleston karibu na Great Yarmouth.  Miili yao ambayo ilikutwa ikiwa imeliwa na ndege wa asubuhi na kufunikwa kwa matope  ilikutwa imetupwa pembeni ya gorofa jirani Breydon.

Jenga Heshima kwa Jamii Kwa kufanya Mambo Haya Matatu

Image
Hakuna ubishi wowote, heshima ni moja ya kitu ambacho karibu kila mtu anakitafuta katika maisha yake. Hakuna mtu ambaye hataki asiwe wa kuheshimika, heshima inatafutwa na watu wengi sana. Ndio maana utakuta kuna watu wanatumia pesa au mbinu nyingi sana kuweza kujenga heshima. Hali hiyo yote inaonyesha kwamba heshima ni mojawapo ya kitu cha thamani na kinachokubalika sana katika jamii yoyote ile. Pamoja na umuhimu wa heshima kwa wengi, sasa kitu ambacho tunatakiwa tujiulize mimi na wewe ni kwamba, je, kati yetu ni wangapi hasa wanajua namna ya kujenga heshima zao katika jamii? Je, pesa peke yake ndio ina uwezo wa kujenga heshima? Au ni kitu gani ambacho unatakiwa uwe nacho ili kikusaifdie kuweza kujenga heshima kubwa katika jamii na kujikuta ukikumbukwa pengine vizazi na vizazi? Kama nia yako ni kutaka kujenga heshima na ukawa mtu wa kuheshimika, fahamu mambo haya;- 1. Toa thamani. Ili uweze kujenga heshima kubwa kwa jamii inayokuzunguka, toa thamani, fanya vi

Dodoma waanza kutenga maeneo ya biashara

Image
MWENYEKITI wa Kamati ya Mipango Miji na Mazingira ambaye pia ni Diwani wa Kikuyu Kusini, Anselm Kutika amesema kata zote za Manispaa za Dodoma zitatenga maeneo kwa ajili ya wafanyabiashara, jambo litakaloondoa tatizo la wafanyabiashara kufanya kazi zao katika maeneo yasiyoruhusiwa. Kutika alisema kata zote za Manispaa ya Dodoma ni lazima zitenge maeneo kwa ajili ya wafanyabiashara ili kuuweka mji katika hali ya usafi. Alitaja sehemu ambazo tayari zimetenga maeneo kwa ajili ya biashara kuwa ni Kisasa, Tambukareli, Kikuyu Kusini, Kizota, Chang’ombe, Nkuhungu, Makole na Kiwanja cha Ndege. “Kamati ya Mipango Miji imepitipisha maeneo kwa ajili ya wafanyabiashara na maeneo hayo yatakuwa kikata na wananchi watakuwa walinzi namba moja,” alisema. Akaongeza, “Kikuyu Kusini tulitoa matangazo kama kuna mtu aliyefikiwa na tangazo na walengwa walikuwa ni wakazi wa kata, hapo awali changamoto ilikuwa baadhi ya D centre zilivamiwa na wakazi wan je ya kata.” Alisema baadh

MANENO YA MWIGULU NCHEMBA, POLISI,VIONGOZI NA 'VILIO VYA WANANCHI' SAKATA LA MAUAJI KIBITI

Image
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, amefanya ziara ya kushtukiza wilayani Kibiti mkoani Pwani na kuteta kwa faragha na askari wa operesheni maalumu ya kuwasaka wauaji. Alisema  mauaji sasa yametosha na Serikali haitikuwa tayari kuona vitendo hivyo vinaendelea   kama ilivyo nchini Somalia. Ziara ya ghafla  imetokana na matukio ya mauaji ya mara kwa mara ya raia katika eneo hilo ambayo yamekuwa yakifanywa na watu wasiojulikana. Akizungumza  wilayani hapa  baada ya kuwatembelea  polisi   katika kambi maalumu ya operesheni ya kusaka wahalifu katika Kata ya Bungu, Mwigulu alisema  Serikali haiwezi kuvumilia mauaji ya mara kwa mara kama yanayotokea Somalia. Waziri alisema serikali  imejipanga kudhibiti hali hiyo kwa sababu kufuga wauaji na wahalifu kuna gharama. “Tunaendelea kufuatilia kazi ambazo mnaendelea kufanya, mapambano ambavyo yameendelea, tuendelee kusonga mbele. “Nikiziangalia takwimu na mwenendo, nazidi kupata maswali n

TABIA 4 ZINAZOHARIBU KINGA ZA MWILI BILA KUJIJUA

Image
Kinga ya mwili ni ile hali ya mwili kuwa na uwezo wa kujikinga wenyewe dhidi ya maradhi mbalimbali.  Mtu anapokuwa na kinga imara za mwili, huepuka kuugua mara kwa mara na kwa kifupi unaweza kusema kwamba kinga ya mwili ndiyo kila kitu katika afya ya binadamu.  Kuumwa mara kwa mara ni dalili tosha kuwa kinga yako ya mwili imeshuka na hivyo unahitaji kuchukua hatua za kuziimarisha. Kwa kawaida Mungu alituumba miili yetu ikiwa na uwezo wa kujikinga na magonjwa yote, laikini mwili utaweza kufanya hivyo endapo tu utapatiwa vyakula vinavyohitaji ili kuimarisha kinga zake. Leo tuangalia aina ya vyakula vya kuepuka ili kuzifanya kinga za mwili kufanya kazi zake vizuri. 1. Mhusika anapaswa kuepuka vyakula vyenye sukari nyingi Sukari siyo nzuri kwa afya yetu hasa inapotumiwa kupita kiwango. Kiwango cha kawaida cha sukari kinachoruhusiwa kutumiwa ni kijiko kimoja kidogo (teaspoon), kinapozidi hapo huwa kinachangia kudhoofisha mfumo wa kinga ya mwili. Inaelezwa kuw

KIGOGO WA SERIKALI ANAYEBANJUKA NA MSANII BATULI HUYU HAPA,MENGI MAZITO YAFICHUKA

Image
UBUYU ulionyooka kabisa umetua kwenye meza ya gazeti hili ukidai kuwa, waziri kijana katika serikali ya Rais Dk.John Magufuli ‘JPM’, amedata kinomanoma na penzi la msanii wa filamu Bongo mwenye shepu bomba, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, Ijumaa lina full stori. Awali zilivuja taarifa kuwa, waziri huyo wa wizara nyeti ambaye ni mume wa mtu (jina lake linahifadhiwa kwa sasa) kafa, kaoza kwa mrembo huyo ambaye ni kada wa CCM na hivyo ameamua kumng’arishia maisha yake ili aweze kumfaidi vizuri. KISIKIE CHANZO “Kama ni kuyapatia maisha, Batuli sasa hivi kayapitia maana mheshimiwa….(anamtaja jina) ndiyo kajiweka kwake sasa hivi, anamhudumia kwa kila kitu, ndiyo maana unamuona mambo yake sasa hivi supa kuliko hata mastaa wengine,” alimwaga ubuyu mtoa habari huyo kisha akaongeza: “Kampangishia mjengo kule Kunduchi na ndinga pia kamnunulia, nyie fuatilieni mtajua ukweli wa ubuyu huu ninaowapa.” IJUMAA KAZINI Baada siri hiyo kuvuja, mmoja wa waandishi wetu alimpigia