Posts

Showing posts from February 10, 2018

BREAKING : ANGALIA MTOTO WA KIUME AFUMANIWA NA BABA YAKE MZAZI CHUMBANI

Image
Kijana mmoja aliyetajwa kwa jina la Dullah, mkazi wa Chamwino, Kibao cha Shule mkoani Morogoro amedaiwa kufumaniwa akijaribu kumlawiti Baba ake mzazi. tukio hilo lakusikitisha lilitokea jumatatu iliyopota usiku nyumbani kwa mzee mmoja maarufu (jina linahifadhiwa kwasababu za kimaadili) anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70. Habari zinasema kijana huyo inadaiwa baada ya kutaka kufanya unyama huo, baba yake alipiga yowe kuomba msaada ambapo baadhi ya wananchi walimwita mwandishi wetu ambaye alipofika eneo la tukio alikuta kundi la wananchi wakijadili, huku mtuhumiwa akiwa amekimbia.

UTAPELI MPYA FEDHA KWENYE SIMU YAKO WATIKISA NCHINI!

Image
IGP Sirro. BADO wizi wa fedha za kwenye mitandao ya simu unaendelea kutikisa nchini ambapo kwa sasa njia mpya imeibuka ambayo unaibiwa fedha kwenye simu yako ukiwa nayo mkononi. Wakizungumza na Risasi Mchanganyiko baadhi ya wananchi walilalamikia utapeli huo na kusema wameibiwa fedha zao ambazo zilikuwa kwenye simu zao. Mmoja wa wananchi hao, Agatha John wa Mwenge jijini Dar alisema aliibiwa fedha zake shilingi 60,000 baada ya kupigiwa simu na mtu ambaye hamfahamu aliyemtaja jina lake kiufasaha na kumdanganya kwamba yeye ni ofisa wa mtandao wa simu anaoweka fedha zake. “Mtu huyo aliniambia kuna zawadi kemkem zitatolewa na mtandao huo kwa wateja ambao wana fedha zaidi ya shilingi 50,000 hivyo alinishauri nimtajie namba yangu ya siri ili fedha na zawadi ziweze kutumwa ndani ya siku tatu,” alisema Agatha. Aliongeza kwamba baada ya kumtajia namba zake za siri aliamini kwamba fedha zake zitakuwa salama kwa sababu simu na kadi yake anayo yeye, hivyo alidhani ...

Nape Nnauye awakomalia usalama wa Taifa

Image
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ameibuka na kuituhumu Idara ya Usalama wa Taifa nchini haifanyi kazi zake ipasavyo inavyohitajika na badala yake wamekalia kusikiliza simu za watu wanavyoongea pamoja na kufanya mambo ambayo hayalindi uchumi wa Tanzania. Nnape ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akichangia bungeni taarifa ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama katika mkutano wa 10 kikao cha nane cha Bunge mjini Dodoma na kuishauri kamati hiyo ipeleke mapendekezo ili waweze kupitia upya sheria ya Usalama wa Taifa na kuiwezesha mikono yao iende mbali, kukumbuka jukumu lao la la kuhakikisha wanalinda uchumi nchi katika kipindi hichi, ambacho demokrasia ya siasa inahama na kuelekea kwenye demokrasia ya uchumi ambapo muda mwingi wanapaswa kuutumia huko na sio pengine. Kutoka na hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Kapteni George Mkuchika amemjibu Nape na wabunge wengine kwamba kazi ya Idara ya Usal...

Hoja ya biashara ya ngono, madanguro yajibiwa na Serikali

Image
Serikali imesema ina andaa mikakati itakayowezesha kudhibiti biashara ya ngono na uwepo madanguro nchini, hasa kwenye maeneo ya mijini. Hayo yamesemwa jana Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile wakati akijibu swali la Mbunge wa Mtambwe, Khalifa Mohammed Issa aliyehoji juu mpango serikali katika kudhibiti biashara ya ngono na madanguro ili kupunguza maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) nchini. Akijibu swali la Issa, Dkt. Ndugulile alisema Serikali inaandaa mikakati mbalimbali ikiwemo utoaji wa elimu kuhusu madhara ya biashara ya ngono kwa jamii pamoja na kuchukua hatua za kisheria kwa wanaojihusisha na baishara hiyo, pamoja na kudhibiti uwepo wa madanguro. Katika hatua nyingine, Dkt. Ndugulile alisema serikali inaendelea kuchukua hatua katika kudhibiti mila na desturi potofu zinazochangia maambukizi mapya ya VVU, ikiwemo ukeketaji na urithishaji wa wajane kwa ndugu w...

Akiwa Safarini, Mbasha Akombwa Kila Kitu Mchana Kweupe

Image
 ALIYEKUWA mume wa Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha akiwa safarini Arusha amekombwa kila kitu na majambazi nyumbani kwake Tabata Kimanga mchana kweupe. Mtu wa karibu na Mbasha aliiambia Mikito Nusunusu kuwa, Mbasha alichanganyikiwa baada ya kurudi na kukuta amekombwa kila kitu cha ndani na majambazi. Baada ya habari hizi kutua kwenye dawati la Mikito Nusunusu, lilimtafuta Mbasha ambaye alikiri kuibiwa kila kitu na kusema kuwa mpaka sasa amesharipoti polisi na uchunguzi bado unaendelea. “Yaani sina la kusema walioniliza wamefanya kazi kwani wamechukua kila kitu cha ndani na kwa kweli wamenirudisha nyuma sana hata sielewi naanzia wapi,” alisema Mbasha. Wakielezea tukio hilo majirani wa eneo hilo walisema kuwa mitaa hiyo mida ya mchana huwa ni tulivu sana kwani watu wengi huwa wanakwenda makazini ndio maana hata majambazi hao wakafanikiwa kuiba kila kitu bila kushtukiwa. “Si unajua nyumba zetu ni za mageti makubwa mtu kujua moja kwa moja kuwa kwa f’lan kaingi...

Akiwa Safarini, Mbasha Akombwa Kila Kitu Mchana Kweupe

Image
 ALIYEKUWA mume wa Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha akiwa safarini Arusha amekombwa kila kitu na majambazi nyumbani kwake Tabata Kimanga mchana kweupe. Mtu wa karibu na Mbasha aliiambia Mikito Nusunusu kuwa, Mbasha alichanganyikiwa baada ya kurudi na kukuta amekombwa kila kitu cha ndani na majambazi. Baada ya habari hizi kutua kwenye dawati la Mikito Nusunusu, lilimtafuta Mbasha ambaye alikiri kuibiwa kila kitu na kusema kuwa mpaka sasa amesharipoti polisi na uchunguzi bado unaendelea. “Yaani sina la kusema walioniliza wamefanya kazi kwani wamechukua kila kitu cha ndani na kwa kweli wamenirudisha nyuma sana hata sielewi naanzia wapi,” alisema Mbasha. Wakielezea tukio hilo majirani wa eneo hilo walisema kuwa mitaa hiyo mida ya mchana huwa ni tulivu sana kwani watu wengi huwa wanakwenda makazini ndio maana hata majambazi hao wakafanikiwa kuiba kila kitu bila kushtukiwa. “Si unajua nyumba zetu ni za mageti makubwa mtu kujua moja kwa moja kuwa kwa f’lan kaingi...

Hatma ya Zitto mikononi mwa Spika

Image
KUADHIBIWA ama kutoadhibiwa na Bunge kwa Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) kuko chini ya Spika Job Ndugai baada ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kukamilisha uchunguzi wa shauri lake. Kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo anakabiliwa na tuhuma za kudharau mamlaka ya Spika kutokana na kauli yake kwamba, "Bunge limewekwa mfukoni na serikali." Akiwasilisha bungeni mjini hapa jana taarifa ya shughuli za Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kipindi cha kuanzia Januari 2017 hadi Januari 2018, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Almas Maige, alisema tayari wameshakamilisha uchunguzi wa shauri hilo. Pia alisema kamati yake imeshamshauri Spika hatua za kuchukua kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge toleo la Januari 2016. Maige ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM), alisema kuwa katika mkutano wa nane wa Bunge, baada ya Spika kupokea na kuikabidhi serikali taarifa za kamati mbili alizoziunda Julai tano kwa ajili ya kufan...