Yanga Yataja Hatma ya Sadney, Lamine na Madeni Yake
Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msolla. MWENYEKI wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msolla, leo Desemba 10, 2019 amezungumzia tetesi za klabu hiyo kutowalipa mishahara wachezaji kwa muda wa miezi miwili na akaweka wazi hatma ya wachezaji Sadney Urikhob na Lamine Moro ambao inasemekana waliandika barua za kutaka kuondoka katika klabu hiyo kwa kutolipwa mishahara yao kwa miezi mitatu. Akiongea na wanahabari alisema ni kweli klabu yake haijawalipa wachezaji mishahara ya miezi miwili ambayo ni Oktoba na Novemba mwaka huu na kwamba iwapo mambo yakienda vizuri watalipwa leo. Aliongeza kwamba habari zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mshambuliaji Sadney Urikhob na beki Moro Lamine, viongozi wamekubaliana kuachana na Sadney na watabakia na Lamine ambaye atalipwa mishahara yake. Akifafanua hali ilivyo klabuni hapo, amesema walipoingia madarakani mwezi Mei 2019 walikuta madeni mbalimbali ikiwa ni pamoja na kudaiwa Sh. milioni 800 na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA)....