A-Z Fumanizi la Shilole, Madee!
Zuwena Mohamed ‘Shilole’. Stori: Gabriel Ng’osha na Sifael Paul YAMEIBUKA tena? Ni takriban mwaka mmoja na ushee tangu skendo ya msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na staa mwenzake wa Bongo Fleva, Hamad Ally ‘Madee’ kudaiwa kufumaniwa na aliyekuwa mpenzi wa Shilole, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ ambapo kila mtu alijitetea kwa upande wake. Shilole na Madee Lakini wikiendi iliyopita, Nuh aliibuka na kuifunua upya skendo hiyo ya kumfumania Shilole laivu akimsaliti na Madee wakiwa hotelini, jambo lililomuuma kila anapokumbuka tukio hilo. Kwa mujibu wa Nuh, aliwakuta wawili hao wakivunja amri ya sita huku mmoja wao akiwa mtupu kama alivyozaliwa. Nuh alidai kuwa hapendi sana kuzungumzia suala lake la uhusiano wa kimapenzi kwani linawafanya watu kusahau muziki wake na kusikiliza mambo mengine nje ya kazi...