Posts

Showing posts from November 29, 2014

BREAKING NEWS: WATU WANNE WAFARIKI KATIKA AJALI YA HELIKOPTA HUKO GOMBO LA MBOTO JIJINI DAR!

Image
Muonekano wa Helikopta eneo la Gonga la Mboto jijini Dar.  Wananchi wakiwa eneo la tukio baada ya Helikopta kuanguka. Helikopta imeanguka leo eneo la Gongo la Mboto, Moshi Bar jijini Dar, kuna watu wanadaiwa kufariki dunia lakini polisi hawajatoa taarifa rasmi juu ya tukio hili.

HATIMAYE LADY JAY DEE AKIRI KUMUACHA MUMEWE GADNER HABASH - MSIKILIZE HAPA

Image
Hatimaye Lady Jaydee amethibitisha kwa kauli yake mwenyewe kuwa ndoa yake na mtangazaji mkongwe wa redio, Gadner G Habash imevunjika. Akiongea leo kwenye Exclusive Friday ya kipindi cha Sunrise cha Times FM, Jaydee amesema ni yeye ndiye aliyeamuacha Gadner. Kwenye mahojiano hayo, Jide alizungumzia kuwa kwenye uhusiano na mtu aliyekuwa akimpiga mara kwa mara licha ya kutomtaja moja kwa moja kuwa ni Gadner lakini alisema alikuwa akiteswa. Kabla ya kuamua kuusema ukweli huo, Jide aliweka wazi kuwa siku zote amekuwa akiepuka kuongea masuala yake binafsi kwenye vyombo vya habari.“Kitu kimoja ambacho ningependa watu wafahamu, mimi sio mtu ambaye huwa napenda kuongea maisha maisha yangu kwenye media, kwenye magazeti au wapi,” alisema. “Na ndio maana lolote ambalo linaendelea ndani ya nyumba yangu au kwenye maisha yangu, sijawahi kulitoa nje. Ni watu wanaongea chochote wanachohisi, chochote wanachotaka kusema.  SOMA ZAIDI>>>>