Haya ndiyo madhara ya kuitana 'Sweet, Dear, Baby' kwenye mapenzi
BABY ni neno la Kiingereza lenye maana ya mtoto, tena mara nyingi linatumika kwa mtoto mdogo. Pia lina maana nyingine ya mpenzi. Ni neno maarufu sana siku hizi; hata wazee kabisa, utasikia wanaitana baby! Mbali na hilo, yapo maneno mengine kama sweet, dear, honey na mengine mengi. Maneno yote hayo ya Kiingereza, yana maana zaidi ya moja, lakini kubwa zaidi ni kumaanisha mpenzi, mpendwa (hutumika katika kuonesha mapenzi ya dhati kwa mwingine). Leo nataka kukupa kitu kipya kabisa kichwani mwako. Unahitaji utulivu wa hali ya juu ili kujifunza hili. Ni maneno mazuri sana, ya kipekee lakini kwa upande mwingine ni hatari kwa sababu hukaribisha matatizo ambayo hayakutarajiwa na mtumiaji. HUTUMIKA WAPI HASA? “Dear, naomba uniamshe saa 12:00 asubuhi, kesho nina vikao vingi sana asubuhi,” inaweza kuwa kauli ya mume akimwambia mkewe, ambaye naye anamjibu: “Sawa sweet, usijali.” Kwa hakika ndipo sehemu sahihi zaidi kutumika. Ni maneno yenye mshawasha mkubwa na huonesha pe