Posts

Showing posts from April 9, 2016

Mambo 8 Muhimu Kuhusu Huduma Mpya ya WhatsApp

Image
KUTOKANA na tatizo la kuingiliwa kwa mawasiliano ya watumiaji wa WhatsApp, hivi karibuni kampuni hiyo ilianzisha huduma ya  end-to-end encryption ili kuboresha huduma zao za mawasiliano hasa katika nyanja ya kuimarisha ulinzi wa mawasiliano ya wateja wao. 1. End-to-end encryption ni nini? Hii ni huduma mpya ya WhatsApp inayotumiwa kwa ajili ya kulinda mawasiliano baina ya mtumaji na mpokeaji kwenye mtandao huo bila mtu wa kati kuingilia mawasiliano hayo. huduma hii pia inapatikana iwapo mtumianji wa ataingiza toleo jipya la WhatsApp. Inatumika kwenye simu zote za iOS na Android. 2. Unawezaje kuwezesha (activate ) huduma hii? Haya yote yanafanyika kwa mfumo kujiendesha wenyewe (automatically), hauhitaji kufanya mpangilio (setting) ili kuwezesha usiri wa mawasiliano yako. 3. Je, huduma hii pia inahusisha upigaji simu wa kwenye WhatsApp call? Ndiyo, kama meseji zako zinalindwa hata WhatsApp calls pia zinalindwa kwa mfumo wa end-to-end encryption ambapo m

SPIKA JOB NDUGAI AKUTANA NA WATAFITI TOKA WASHINGTON DC-MAREKANI.

Image
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kulia) akizungumza na Bwana Tye Ferrell kutoka Shirika la Utafiti la Tetra Technology lililopo nchini Washington DC Marekani, pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mkandala (katikati) wakati walipomtembelea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam 08 Aprili, 2016. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kulia) akimweleza jambo Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mkandala (katikati) wakati wa mazungumzo katika ofisi ya Mhe. Spika jijini Dar es Salaam leo 08 Aprili, 2016. Mtafiti toka Shirika la Utafiti la Tetra Technology lililopo nchini Washington DC Marekani Bwana Tye Ferrell akimweleza jambo Mhe. Spika Job Ndugai (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo katika ofisi ya Mhe. Spika jijini Dar es Salaam leo 08 Aprili, 2016. Watafiti kutoka Shirika la Utafiti lililopo Washington DC-Marekani Bwana Patrick McGoven (kushoto

Dkt. Shein Atangaza Baraza Lake la Mawaziri

Image
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dkt. Ali Mohamed Shein RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dkt. Ali Mohamed Shein leo Jumamosi, April 9, 2016 ametangaza Baraza la Mawaziri litakalosimamia kazi za serikali kwa kipindi cha uongozi wake wake kwa mujibu wa sheria. Dkt. Shein amesema amepunguza ukubwa wa baraza hilo kutoka wizara 16 hadi kuwa wizara 13 zenye Mawaziri ni 13 na Manaibu waziri 7, ambapo wizara tatu amezivunja na kuzigawa ndani ya hizo wizara 13 za sasa. Ameongeza kuwa, mawaziri aliowatangaza leo atawaapisha kesho Jumapili asubuhi katika Viwanja vya Ikulu visiwani Zanzibar. Baraza la Mawaziri Zanzibar hao ni; 1). Ofisi ya Rais na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi – Issa Haji Ussi Gavu. 2). Katiba na Sheria Utumishi wa Umma – Haroun Ali Sleiman. 3). Tawala za Mikoa na Idara maalum – Haji Omari Kheir. 4). Makamo wa 2 wa Rais – Mohd Aboud. 5). Waziri wa Fedha na Mipango – Dk. Khalid Salum Mohd. 6). Afya – Mahmoud Thabit Kombo. 7)

SHAMSA FORD AMSEKWA RUMANDE MZAZI MWENZIE,MAZITO YAFICHUKA

Image
Staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford. NA IMELDA MTEMA, Risasi Jumamosi STAA wa filamu Bongo, Shamsa Ford juzikati amemsweka lupango mzazi mwenziye Dick Matoke, katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa kile kinachodaiwa kuwa mzazi mwenzake huyo kuwa na tabia ya kumtukana mara kwa mara akishirikiana na mpenzi wake wa sasa ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja. Kwa mujibu wa chanzo makini, Dick na mwanamke wake wa sasa wamekuwa wakimtumia meseji za matusi Shamsa kitendo ambacho mwigizaji huyo alikuwa akikivumilia lakini katikati ya wiki hii, uvumilivu ukamshinda, akaamua kwenda kumshtaki. “Yaani hakuna kitu ambacho Shamsa alikuwa hakipendi kama kutumiwa meseji na mzazi mwenzake huyo na mwanamke wake zikimtusi kwa maana alivumilia mpaka akachoka, akaona bora aende polisi kumshtaki,” kilisema chanzo.   Shamsa Ford enzi akiwa na mzazi mwenziye Dick Matoke.   Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa, baada ya kwenda polisi na kufungua mashtaka yaliyosomeka; OB/RB/6522/2

SABABU ZA RAIS MAGUFULI Kwanini Hapendi Sana Kusafiri Nje ya Nchi

Image
Tunajua Rais Magufuli amekuwepo nchini Rwanda kwa ziara ya siku mbili kuanzia April 6 2016 mpaka April 7 jioni aliporudi Tanzania, kwenye moja ya maongezi yake mbele ya Wananchi wa Rwanda ameongea pia kuhusu kwanini hapendi kusafiri nje ya nchi na toka achaguliwe October 2015, amesafiri nje ya nchi kwa mara ya kwanza April 2016. ‘Nataka niwaeleze ndugu zangu, mimi sipendi sana kusafiri kwasababu ninapenda kubana matumizi… nimealikwa sehemu nyingi nimealikwa Ulaya lakini na sehemu nyingine bado sijaenda, nilipoalikwa na Muheshimiwa Kagame nimekuja na ninataka niwaeleze ndugu zangu wa Rwanda hii ndio safari yangu ya kwanza kutoka nje ya Tanzania‘ – Rais Magufuli" .

DIAMOND PLATINUMS YAMKUTA MAZITO,MASHEHE WAMJIA JUU,GUMZO KILA KONA

Image
  NA mwandishi wetu, Risasi Jumamosi Dar es Salaam: Kitendo cha kuposti picha inayomuonesha akiwa ametoboa pua na kuvaa kipini kilichofanywa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kimemfanya yamkute mazito kufuatia mashehe kumjia juu na kuwa gumzo. Gumzo lilianza juzikati baada ya Diamond kutupia picha kwenye akaunti yake ya Instagram, ikimuonesha akiwa amevaa kipini, kama wafanyavyo wanawake, kitendo kilichoamsha mjadala mkubwa kwa mashabiki na wadau mbalimbali wa muziki wake. Wapo waliomuunga mkono kwa maelezo kwamba hakuna mtu anayepaswa kumuingilia kwa sababu hayo ni maisha yake binafsi, huku wengine wakienda mbele kwa kuwatolea mfano mastaa wengine wakubwa duniani kama Chris Brown, Wiz Khalifa, marehemu 2Pac na wengineo kwamba nao waliwahi au wametoboa pua. Hata hivyo, kundi jingine kubwa, lilimjia juu msanii huyo na kumtaka kuacha kuiga mambo yanayofanywa na wasanii wa Ulaya na Marekani na badala yake, awe kioo cha jamii kwa kuenzi na kudumisha

KUHUSU SAKATA LA WALIMU KUANZA KUVAA SARE,WIZARA YA ELIMU YATOA UFAFANUZI HUU..!!

Image
WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imekanusha taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa Waziri wake Profesa Joyce Ndalichako ametaka walimu kuandaliwa sare. Taarifa iliyotolewa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini inasema kuwa taarifa hizo si za kweli na kuwaonya watu wanaotoa taarifa za uzushi kuacha mara moja. Imesema imejipanga kuhakikisha inachukua hatua za kisheria kwa watakaobainika kuanzisha na kueneza uzushi huu. “Tunapenda kuufahamisha umma kuwa taarifa hizi si za kweli. Watu wanaoeneza taarifa za kizushi za aina hii waache kufanya hivyo ili kuepusha usumbufu unaojitokeza,” ilisema taarifa hiyo. Taarifa zilizokuwa zimeenea kwenye mitandao zinasema kuwa Profesa Ndalichako amesema nguo kwa ajili ya walimu zinaandaliwa ambazo zitakuwa aina tatu. Sare hizo zitakuwa ni mashati matatu meupe yenye nembo ya taifa, suruali na sketi zitakuwa za rangi ya bluu, kijani na kaki na kofia yenye nembo ya taifa. Ilidai mwongoz

KIGOGO WA WEMA SEPETU NA KAJALA ,CK ANASWA LIVE AKICHOMA NA KUUZA MISHIKAKI

Image
Dar es Salaam: Upepo umebadilika! Aliyekuwa kigogo serikalini katika idara nyeti kabla ya ‘kutumbuliwa’ na kufikishwa  Mahakama ya Kisutu jijini Dar kwa tuhuma za kughushi hundi na kujichotea fedha kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu ambaye aliwahi kudaiwa kuwa mwandani wa staa wa Bongo, Wema Isaac Sepetu, Clement Kiondo ‘CK’ au Kigogo wa Wema amenaswa laivu akichoma na kuuza mishikaki. RISASI JUMAMOSI LAPEWA ‘UBUYU’ Hivi karibuni, Gazeti la Risasi Jumamosi lilipokea simu kutoka kwa chanzo chake kikisema CK ziku hizi anauza mishikaki. Mazungumzo yalikuwa hivi… Chanzo: “Haloo…naongea na Risasi Jumamosi hapo?” Risasi Jumamosi: “Ndiyo…karibu, tukusaidie nini?” Chanzo: “Hivi mna habari kuwa yule Kigogo wa Wema. Mnamuita CK, siku hizi anatuhudumia mishikaki baa?” Risasi Jumamosi: “Lakini sisi hatuoni tatizo. Kwani ni yake au anamsaidia mtu? Na ni sehemu gani?” Chanzo: “Hakuna tatizo lakini sasa amekuwa gumzo. Hebu fikirieni alivyokuwa na Wema na Kajala (Masanja) alikuwa a