Posts

Showing posts from May 13, 2016

Kassimu Majaliwa Akutana na Viongozi Mbalimbali, London Uingereza

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga (kulia) wakizungumza na Waziri  Mkuu  wa Norway, Erna  Solberg katika  Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika London Uingereza, May 12, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na  Waziri  Mkuu  wa Norway, Erna Solberg katika  Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016.  Kulia ni  Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga (wapili kushoto) wakizungumza na Waziri  Mkuu  wa Norway, Erna  Solberg (kulia) katika  Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na...

Picha za Waziri wa Sudan Zazua Gumzo Mtandaoni.

Image
Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Sudan Kusini Mh. Mabior Garang De Mabior ambaye ni mtoto wa Rais wa kwanza wa Sudan Kusini na kiongozi wa zamani wa kikundi cha waasi cha SPLA/M cha Sudan Dr. John Garang amekuwa gumzo mitandaoni baada ya picha zake zenye utata kusambaa katika mitandao ya kijamii. Mabior Garang ambaye ni mtoto mkubwa wa Marehemu John Garang ambaye aliongoza kikundi cha waasi kwa muda mrefu kabla ya kufariki katika ajali ya Helkopta mwaka 2005 akiwa Rais wa Sudan Kusini, alifukuzwa katika kikao cha Baraza la mawaziri na Rais wa nchi hiyo Salva Kiir kwa kile kilichosemwa kuvaa mavazi yasiyostahili. Mwaka 2014, Mabior aliwahi kukamatwa na maafisa usalama wa Ethiopia kwa kile kilichohisiwa kuwa jaribio la kutaka kumuua Rais wa sasa wa Sudan Kusini Salva Kiir baada ya kukamatwa akiwa hotelini na bastola ikiwa na risasi sita. Baada ya kukamatwa na kuhojiwa alisema alitaka kukutana na Rais Kiir kwani ameharibu kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na Baba yake J...

Rais Magufuli alivyofanya ziara ya kushtukiza uwanja wa ndege Dar es salaam

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua mara moja dhidi ya dosari za ukaguzi zilizopo katika kitengo cha ukaguzi wa mizigo na abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ( Terminal One ) Dar es salaam. Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 13 Mei, 2016 alipofanya ziara ya kushtukiza katika uwanja huo na kubaini kuwa mashine za ukaguzi za sehemu ya kuwasili abiria na mizigo hazifanyi kazi kwa muda mrefu. Maafisa wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere waliokuwa wakitoa maelezo juu ya hali ya kitengo cha ukaguzi wa mizigo na abiria katika uwanja huo, walikuwa wakitoa taarifa zinazotofautiana kuhusu utendaji kazi wa mashine za ukaguzi, hali iliyosababisha Dkt. Magufuli aamue kuiagiza wizara husika kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua mara moja. “ Unajua mimi sipendi kudanganywa, ni...

Sumaye ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu Chadema

Image
  Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye. Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Mwenyekiti wa CHADEMA – Taifa, Freeman Mbowe amekiambia Kikao cha Kamati Kuu jana kuwa, anampendekeza Sumaye kuwa mjumbe wa CC kwa lengo la kuimarisha chama hicho. Amesema, dhamira ya CHADEMA ni kujiimarisha kwa ajili ya uchaguzi ujao, kwa kutumia kila mwanachama kufanya kazi ya uenezi. Kamati Kuu imeridhia uteuzi wa Sumaye kuwa mjumbe wa Kamati Kuu. Naye Sumaye amemshukuru Mbowe kwa kumteua kushika nafasi hiyo na kuahidi kukitumikia chama hicho kwa nguvu zake zote.

GIGY MONEY AMETAJA HII LIST YA MA-STAR WAKUBWA BONGO TAYARI AMETOKA NAO KIMAPENZI.

Image
Msanii Na Video Queen Gigy Money amefunguka leo kwenye Planet bongo ya East Africa radio kwamba ameshatembea na Ali Kiba, Rich Mavoko na Hemed PhD kwa nyakati tofauti na wote walimtongoza kwenye mtandao wa instagram. Gigy Money amesema kwa sasa amefunga Dm yake instagram sababu ya kuondoa usumbufu wa wanaume wanaomtaka kila leo. Kwa sasa amepata sponsor anaempa pesa nyingi almost laki 5 kila siku hivyo hana mpango wa kupata bwana mwingine labda atokee mwenye hela zaidi.

JPM Aondoka Kampala… Kurejea Tanzania

Image
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Kikundi cha ngoma za asili cha Entebe nchini Uganda wakati akiondoka kurejea nchini.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipita mbele ya gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili ya kumuaga katika uwanja wa ndege wa Entebe wakati akiondoka kurejea nyumbani Tanzania.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa makofi na baadhi ya  viongozi mbalimbali wakati alipowasili kwenye hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa Viongozi wakuu wanchi mbalimbali siku walipowasili Kampala nchini Uganda. Waandishi mbalimbali wa Habari kutoa nchi tofauti wakiwa na shauku ya kupata picha ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kumalizika kwa sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Museveni zilizofanyika kwenyeuwanja wa Uhuru wa ...