Jaji Mutungi Avifutia Usajili Vyama Vitatu vya Siasa Nchini
DAR ES SALAAM: Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi leo amevifutia usajili wa kudumu vyama vitatu vya siasa kwa makosa mbalimbali. Vyama hivyo vilivyofutwa ni pamoja na Chama cha Haki na Ustawi wa Jamii (CHAUSTA) kinachoongozwa na James Mapalala, Chama cha The African Progressive Party of Tanzania (APPT Maendeleo) kinachoongozwa na Peter Kuga Mziray na Chama cha Jahazi Asilia kilichokuwa kinaongozwa na Kassim Bakari Ally. Akiongea na wanahabari leo, Jaji Mutungi amesema amevifuta vyama hivyo kwa kutumia kifungu cha 19 cha sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992. Jaji Mtungi ameongeza kuwa, mchakato wa kufuta usajili wa vyama hivyo unatokana na zoezi la uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa mengine ya sheria ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu lililofanyika kuanzia Juni 26 hadi Julai 2016. Katika zoezi hilo la uhakiki ilibainika kuwa vyama tajwa hapo juu vimepoteza s...