Breaking News: Winnie Mandela afariki dunia
Winnie Mandela, mke wa zamani wa Nelson Mandela, ambaye pia alipigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini amefariki dunia akiwa na miaka 81. Habari za kifo chake zimethibitishwa na msaidizi wake. Winnie alizaliwa mnamo 26 Oktoba mwaka 1936, na ingawa yeye na mumewe - Nelson Mandela - walitalikiana mapema miaka ya 1990, Winnie Madikizela Mandela kama alivyofahamika rasmi alisalia kutoa mchango katika maisha ya Bw Mandela. Alikuwepo na walishikana mikono alipokuwa akiondoka gerezani baada ya kufungwa kwa miaka 27. Lakini maisha yake pia yalikumbwa na utata. Winnie alikuwa na miaka 20 hivi pale alipojipata katika siasa. Alisomea kazi ya utoaji huduma za kijamii na haraka aliyazoea maisha ya kuwa mama na mwanasiasa. Kujitolea kwakena ukakamavu wake vilionekana mumewe alipofungwa jela maisha mwaka 1964 na akaachwa kuendeleza harakati za kisiasa. "Kamwe sitakata tamaa na watu wangu hawatapoteza matumaini kamwe, bila shaka tunatarajia kwamba kazi...