RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO MADOGO YA WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI


1 (12)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 13 Agosti, 2018 amefanya uteuzi wa Mkuu wa Wilaya 1, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji 41, na amewahamisha vituo vya kazi Mkuu wa Wilaya 1 na Wakurugenzi wa Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji 19.
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 13 Agosti, 2018 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa Mhe. Dkt. Magufuli amemteua Bi. Senyi Simon Ngaga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mkoa wa Mwanza.
Bi. Senyi Simon Ngaga amechukua nafasi ya Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato Mkoani Geita, baada ya Mkuu wa Wilaya ya Chato aliyeteuliwa hivi karibuni Kanali Patrick Norbert Songea kwenda kwenye mafunzo ya kijeshi nje ya nchi.
Uteuzi wa Bi. Senyi Simon Ngaga unaanza leo tarehe 13 Agosti, 2018 na Wakuu wa Wilaya wote wawili wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi mara moja.
AIDHA, Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi na uhamisho wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji, kufuatia baadhi ya Wakurugenzi waliokuwa katika nafasi hizo kustaafu, kupangiwa kazi nyingine, kuhamishwa na wengine kuondolewa katika nafasi za ukurugenzi kama ifuatavyo;
  1. 1.   Mkoa wa Arusha.
                        i.         Jiji la Arusha – Dr. Maulid Suleiman Madeni.
                       ii.         Halmashauri ya Wilaya ya Meru – Bw. Emanuel Mkongo.

  1. 2.   Mkoa wa Dar es Salaam.
                        i.         Manispaa ya Temeke – Bw. Lusubilo Mwakabibi (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma).
                       ii.         Manispaa ya Ubungo – Bi. Beatrice Dominic Kwai (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara).
                     iii.         Manispaa ya Ilala – Bw. Jumanne Kiango Shauri (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Korogwe).
                     iv.         Manispaa ya Kigamboni – Bw. Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa).

  1. 3.   Mkoa wa Dodoma.
                        i.         Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa – Bw. Mustafa S. Yusuph.
                       ii.         Halmashauri ya Mji wa Kondoa – Ndg. Msoleni Juma Dakawa.
                     iii.         Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa – Bw. Paul Mamba Sweya.
                     iv.         Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa – Dkt. Omary A. Nkullo.

  1. 4.   Mkoa wa Geita.
                        i.         Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale – Bi. Mariam Khatib Chaurembo.
                       ii.         Halmashauri ya Wilaya ya Chato – Bw. Eliud Leonard Mwaiteleke (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi).

  1. 5.   Mkoa wa Iringa.
                        i.         Halmashauri ya Manispaa ya Iringa – Bw. Hamid Ahmed Njovu (amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga).
  1. 6.   Mkoa wa Kagera.
                        i.         Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi – Bw. Innocent Mbandwa Mukandala.
                       ii.         Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba – Bw. Limbe Bernard Maurice (amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi).
                     iii.         Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba – Bw. Solomon O. Kimilike.

  1. 7.   Mkoa wa Katavi.
                        i.         Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo – Bw. Ramadhan Mohamed.

  1. 8.   Mkoa wa Kigoma.
                       ii.         Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma – Ndg. Mwailwa Smith Pangani (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo).
                     iii.         Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko – Ndg. Masumbuko Stephano Magang’hila.
                     iv.         Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma – Bi. Upendo Erick Mangali.

  1. 9.   Mkoa wa Kilimanjaro.
                        i.         Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga – Ndg. Zefrin Kimolo Lubuva.
                       ii.         Halmashauri ya Wilaya ya Moshi – Tatu Selemani Kikwete (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha).

  1. 10.                  Mkoa wa Lindi
                        i.         Halmashauri ya Wilaya ya Liwale – Bw. Nassib Bakari Mmbaga (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Temeke).
                       ii.         Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa – Bw. Renatus Blas Mchau.




  1. 11.                  Mkoa wa Mara.
                        i.         Halmashauri ya Wilaya ya Musoma – Bw. Kayombo Lipesi John (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo).
                       ii.         Halmashauri ya Wilaya ya Butiama – Ndg. Magori Mgalani Alphonce.

  1. 12.                  Mkoa wa Mbeya.
                        i.         Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya – Bw. Stephan Edward Katemba (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni).
                       ii.         Halmashauri ya Jiji la Mbeya – Mrakibu Mwandamizi wa Polisi  James Cola Kasusura.
                     iii.         Halmashauri ya Wilaya ya Kyela – Bi. Lucy L. Mganga.

  1. 13.                  Mkoa wa Morogoro.
                        i.         Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero – Mhandisi Stephano Bulili Kaliwa.
                       ii.         Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro – Ndg. Kayombe Masoud Lyoba.
                     iii.         Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi – Bw. Mussa Elias Mnyeti.
                     iv.         Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa – Asajile Lucas Mwambambale.

  1. 14.                  Mkoa wa Mtwara.
                        i.         Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara – Kanali Emmanuel Hally Mwaigobeko.

  1. 15.                  Mkoa wa Mwanza.
                       ii.         Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi – Ndg. Kisena Magena Mabuba.
                     iii.         Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe – Bi. Ester Anania Chaula.


  1. 16.                  Mkoa wa Njombe.
                        i.         Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe – Ndg. Edes Philip Lukoa (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze).
                       ii.         Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa – Ndg. Sunday Deogratius George.

  1. 17.                  Mkoa wa Pwani.
                        i.         Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze – Bi. Amina Mohamed Kiwanuka (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe).
                       ii.         Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha – Ndg. Butamo Nuru Ndalahwa (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Moshi).

  1. 18.                  Mkoa wa Rukwa.
                        i.         Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi – Bw. Engelus Wilbard Kamugisha.
                       ii.         Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo – Ndg. Msongela Nitu Palela (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala).
                     iii.         Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga – Bw. Jacob James Mtalitinya (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Nzega).

  1. 19.                  Mkoa wa Ruvuma.
                        i.         Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga – Bw. Juma Ally Mnwele.
                       ii.         Halmashauri ya Mji wa Mbinga – Bi. Grace Stephen Quintine.
                     iii.         Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo – Bw. Evans Nachimbinya.
                     iv.         Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru – Bw. Gasper Zahoro Balyomi.


  1. 20.                  Mkoa wa Shinyanga.
                        i.         Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga – Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Hoja Mahiba.

  1. 21.                  Mkoa wa Simiyu.
                        i.         Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi – Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto James Marco John Mtembelea.

  1. 22.                  Mkoa wa Singida.
                        i.         Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi – Bw. Justice K. Lawrence

  1. 23.                  Mkoa wa Songwe.
                        i.         Halmashauri ya Wilaya ya Tunduma – Mhandisi Mussa Natty.
                       ii.         Halmashauri ya Wilaya ya Songwe – Bi. Fauzia Hamidu.
                     iii.         Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi – Ndg. Kazimbaya Makwega. Adeladius (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto).

  1. 24.                  Mkoa wa Tabora.
                        i.         Halmashauri ya Wilaya ya Nzega – Ndg. Sekiete Seleman Yahaya.
                       ii.         Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge – Bi. Martha Daudi Luleka.

  1. 25.                  Mkoa wa Tanga.
                        i.         Halmashauri ya Mji wa Korogwe – Bw. Nicodemus John Bee.
                       ii.         Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi – Ndg. Gracia Max Makota.
                     iii.         Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli – Bw. George Haule.
                     iv.         Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe – Ndg. Kwame Andrew Daftari.
                       v.         Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto – Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Ikupa Harrison Mwasyoge.
Wakurugenzi ambao katika mabadiliko haya wamebadilishiwa vituo vya kazi wanapaswa kwenda kuripoti katika vituo vyao vipya vya kazi mara moja, na Wakurugenzi ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza wanatakiwa kuripoti kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Jijini Dodoma siku ya Jumatano tarehe 15 Agosti, 2018 kwa ajili ya kupata maelekezo zaidi kuhusu majukumu yao na kula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma.
Wakurugenzi wateule wanaokwenda TAMISEMI Jijini Dodoma wanapaswa kuwa na vyeti vyao halisi (Originals), pamoja na nakala za vyeti hivyo zilizothibitishwa kisheria (Certified Copies) vinavyoonesha matokeo ya kumaliza elimu ya kidato cha nne, kidato cha sita na elimu ya taaluma walizosomea.
Wakurugenzi ambao vituo vyao vya kazi havikutajwa katika mabadiliko haya wanaendelea na nyadhifa zao katika vituo walivyopo.
WAKATI HUO HUO, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Huruma Mkuchika amemteua Ndg. Mnkondo Yesaya Bendera kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Rungwe ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Moses Maurus Mashaka ambaye amepangiwa kazi nyingine.
Bw. Bendera anatakiwa kuripoti kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jijini Dodoma Jumatano tarehe 15 Agosti, 2018 kwa maelezo zaidi, akiwa na vyeti vyake halisi (Originals) vya elimu ya Sekondari na vya elimu yay a taaluma alizosomea.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
13 Agosti, 2018

Comments

Popular posts from this blog