Posts

Showing posts from January 3, 2015

DEREVA TEKSI AFUMANIWA, AUAWA KWA KUCHOMWA KISU KIFUANI

Image
DEREVA teksi Hamis Seleman (18), mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam, amekufa baada ya kuchomwa kisu kifuani na Ali Kimodo, aliyemfumania akiwa na mpenzi wake. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Mary Nzuki alisema tukio hilo lilitokea usiku wa saa 9:00 wa kuamkia mwaka mpya, katika eneo la Vingunguti mtaa wa Magenge, ambapo Seleman alifumaniwa na msichana mmoja (jina tunalihifadhi), mwenye umri wa miaka 15, mkazi wa Tabata. Nzuki alisema kuwa baada ya tukio hilo kutokea, Kimodo pamoja na binti huyo walitoroka, hivyo polisi inaendelea na upelelezi kwa ajili ya kuwapata watu hao. Aliongeza kuwa katika maeneo mengine ya mkoa huo, hali ilikuwa shwari katika sherehe hizo za sikukuu ya Mwaka Mpya. Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kihenya Kihenya alisema hali ilikuwa shwari katika eneo lake, kuanzia Krismasi na Mwaka Mpya. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillus Wambura alisema katika eneo lake, pia hakukuwa na tukio lolote kubwa la u...

PICHA ZA BAADHI YA WAKE WA MFALME MSWATI>>EBWANA JAMAA ANAJUA KUCHAGUA

Image
Meet some of KING MSWATI's wives, Very Hot, the Guy must be lucky

KUNDI LA PANYA ROAD LATIKISA DAR JANA

Image
KIKUNDI kinachodaiwa kuwa Panya Road kimetikisa maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kwa kupora mali, kujeruhi watu na kuzua sintofahamu katika maeneo ya jiji hilo wakiwa na mapanga mikononi. Maeneo yaliyokumbwa na dhooruba hiyo ni pamoja na Sinza, Tandale, Mwananyamala na maeneo mengineyo usiku huu. Maduka na baa zimefungwa na kupelekea polisi kupiga risasi hewani kuwatawanya watu waliokuwa wamekaa kimakundimakundi. Imeelezwa kuwa fujo zilianzia mchana leo baada ya kiongozi wa Panya Road aitwaye Diamond kuuawa maeneo ya mpakani mwa Tandale na Mwananyamala darajani usiku wa kuamkia mwaka mpya  kwa kukatwakatwa na mapanga . Baada ya kumzika mwenzao leo, vijana hao wakajipanga kwa ajili ya kufanya fujo. Usiku ulipoingia wakaanza kazi na kusababisha taharuki kwa wakazi wa Jiji la Dar. Baadhi ya mashuhuda walioshuhudia matukio hayo wanadai vijana hao walikuwa na silaha mbalimbali yakiwemo mapanga na walivamia maeneo kadhaa zikiwemo baa. Wat...

JOKATE KIDOTI AFUNGUKA KUHUSU SIRI ZA KUTOMASWA KIMAPENZI!

Image
Mwanamitindo ambaye pia ni msanii wa filamu Bongo, Jokate Mwegelo. MWANAMITINDO ambaye pia ni msanii wa filamu Bongo, Jokate Mwegelo amesema kuwa hapendi kuigiza sini za mapenzi hasa zile anazotakiwa kushikwashikwa na mwanaume hasa asiyemjua.Jokate alifunguka hayo wakati paparazi wetu alipotaka kujua namna ambavyo wazazi na mpenzi wake wanavyolipokea suala la yeye kuigiza sini za kushikwashikwa na wanaume tofauti katika filamu ndipo alipofunguka kuwa suala hilo limekuwa likipigwa vita na wazazi wake lakini analazimika kufanya kwa sababu ndiyo kazi aliyoichagua. Jokate Mwegelo akipozi. “Wazazi wangu wanachukia sana jambo hili na huwa wanasema bora niache filamu, hata mimi mwenyewe huwa sipendi ila huwa navumilia kwa kuwa ni kazi, sina jinsi,” alisema Jokate.

RAIS AMTEUA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI MPYA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Uteuzi wa Bwana Masaju ulianza jana, Ijumaa, Januari 2, 2015 na ataapishwa keshokutwa, Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam.Kabla ya uteuzi wake, Bwana Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana Masaju pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, DAR ES SALAAM. 3 Januari, 2015 

MUME AMLIPUA KWA PETROL MKE WAKE BAADA YA KUKATAA KUPASHA MOTO CHAKULA

Image
Matuko ya kupiga na kunyanyaswa wanawake bado yameendelea kuchukua nafasi katika nchi malimbali za Afrika. Tumekuwa tukiona ripoti mbalimbali za matukio mabaya ya unyanyasaji, kutoka Kenya mwanaume mmoja amefunguliwa mashtaka baada ya jaribio la kutaka kumuua mke wake kwa madai alishindwa kumpatia chakula cha moto. Mwanaume huyo Peter Muthii alimmwagia mkewe petrol akiwa amelala, akawasha moto na kumfungia ndani ambapo muda mfupi baadaye majirani walikuja kumwokoa na kumkimbiza hospitali. Kisa cha tukio hilo kimetajwa kuwa ni baada ya mwanaume huyo kurudi nyumbani usiku na kumtaka mkewe kumpashia chakula lakini mkewe alimwambia apashe mwenyewe kitendo kilichomkwaza, akaamua kumlipua kwa kutumia petrol iliyokua chini ya kitanda chao.