Posts

Showing posts from January 8, 2018

Lowassa, Mbowe wamtembelea Kingunge Hospitali

Image
Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ameongozana na Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Edward Lowassa kumjulia hali Mzee Kingunge Ngumbare Mwiru aliyelazwa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili anapopatiwa matibabu. Mzee Kingunge anatibiwa majeraha baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake . Hivi karibuni Rais John Magufuli alifika hospitalini hapo kumjulia hali Kingunge ambaye ni miongoni mwa wazee wakongwe kwenye siasa za Tanzania ambaye amewahi pia kushika nyadhifa mbalimbali Serikalini tangu awamu ya kwanza hadi ya nne.

RAIS MAGUFULI AANIKA MADUDU ZAIDI WIZARA YA MADINI

Image
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameanika madudu mengine ya Wizara ya Madini akisema kuwa baadhi ya wateule wake katika wizara hiyo wamekuwa wazembe katika kutekeleza maagizo na kutimiza majukumu yao kama watendaji wa serikali. Magufuli ameyasema hayo leo Jumatatu wakati akimwapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais ametolea mfano wa sheria mpya ya madini iliyopitishwa bungeni mwezi Julai mwaka jana, ambapo amesema mpaka sasa wizara hiyo haijapitisha kanuni (regulations) ili sheria hiyo iweze kufanya kazi jambo ambalo amesema ni uzembe usiovumilika huku akimwagiza Waziri wa Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi kukamilisha kanuni hizo na kuzisaini kufikia Ijumaa ya wiki hii. “Nakushukuru Mhe spika kwa kutoa ushauri kwa serikali na sisi tumekuwa tukiufuata sana. Wizara ya madini ina changamoto sana na hata sasa ina changamoto na haifanyi kazi vizuri. Spika utakumbuka mwezi wa saba mlifany

RAIS ABAINI MADUDU TENA BANDARINI, ATEUA KAMISHNA WA MADINI

Image
RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Shukrani Elisha Manya Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) kuwa Kamishna wa Madini. Rais ametangaza uteuzi huo leo Jumatatu Januari 8, 2018 alipokuwa akitoa hotuba fupi mara baada ya kumuapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini. Nimesikia tatizo ni kamishna wa madini, sasa nimeamua kumteua kamishna mpya wa madini, jina lake linaanza na Prof. Shukrani Elisha, huyo atakuwa ndiye mtendaji na msimamizi mkuu wa madini. Mambo ya hovyo ni mengi mno, nilipotembelea bandarini niliunda katume kasirisiri hivi, kwa kulihusisha Jeshi la Wananchi, TISS na Polisi. Yanayogundulika huko ni ya ajabu, kuna hadi simenti za zamani sana, yapo makontena bandarini na pale Ubungo. Mimi sio mwanasiasa mzuri wa kubembelezabembeleza, nikitoka mimi mtapata wakubembeleza, ila mimi nataka kabla ya Ijumaa regulations (kanuni za sheria ya madini) ziwe zimesainiwa. Pro Kabudi nendeni mkazifanyie kazi, tafuta watu wa kukusaid

BREAKING NEWS: NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARALA LA NNE

Image
BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mitihani ya upimaji wa darasa nne na kidato cha pili iliyofanyika Novemba mwaka jana, huku idadi kubwa ya wanafunzi wakifaulu vizuri katika mitihani hiyo. Akitangaza matokeo hayo leo Jumatatu, Januari 8, Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde amesema jumla ya wanafunzi 1,086,156 waliofanya mtihani wa darasa la nne wamefaulu kati ya 1,158,444 waliofanya upimaji huo. Amesema wanafunzi hao wamefaulu kwa kupata alama zenye madaraja ya A,B,C na D wakati wanafunzi 72,288 sawa na asilimilia 6.24 wamepata alama za daraja E, ambao ni ufaulu usioridhisha. Kuhusu matokea ya upimaji wa kidato cha pili, Dk Msonde amesema jumla ya wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 82.32 kati ya 486,742 waliosajiliwa kufanya mtihani huo wamepata ujuzi wa maarifa ya kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu. Dk Msonde alisema wanafunzi wa kidato cha pili 51,807 sawa na asilimia 10.68 wameshindwa kupata alama za kuwaweze