Posts

Showing posts from September 2, 2013

Nimepewa majina ya wabunge wauza dawa za kulevya: Wamo CCM, Chadema

Image
Mbunge wa Nzega (CCM), Dk. Khamis Kigwangallah, amesema amepokea majina ya wabunge, viongozi wa serikali na wafanyabiashara maarufu nchini ambao ni mapapa wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya. Hata hivyo, Dk. Kigwangallah ambaye amepania kuwataja bungeni watu wanaojihusisha na biashara hiyo haramu, amesema baada ya kukabidhiwa majina hayo kutoka kwa wananchi, anafanya uchunguzi na kupata ushahidi ili kujiridhisha kabla hajachukua hatua ya kuwataja. Miongoni mwa majina ya wabunge aliyopewa wamo kutoka CCM na Chadema, na wafanyabiashara maarufu wote wanatoka mkoa wa Dar es Salaam. "Nawashukru wananchi wamenipa ushirikiano hadi jana wamenikabidhi majina ya watu saba ambao ni wabunge wawili, kiongozi mmoja mwandamizi wa serikali na wafanyabiashara wanne, ambao wote ni mapapa wauza unga na siyo madagaa," alisema Dk. Kingwangallah. Alisema katika kuhakikisha anatekeleza alichoahidi amemwandikia barua Spika wa Bunge kumuomba atoe maelezo

Kumbukumbu Ya Kuawa Kwa Mwangosi Na Swali La Mtoto Yule...

Image
Ndugu zangu, HUWEZI kutawala miili ya watu ukaacha mioyo yao. Ndiyo, mjumbe hauawi, ni kauli ya hekima ya tangu enzi za wahenga wetu. Leo ni mwaka mmoja tangu mwandishi wa habari na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wandishi wa Habari mkoani Iringa, Daud Mwangosi kuawa. Ilikuwa ni Jumapili ya Septemba 2, 2012. Hakika, siku ile itabaki katika kumbukumbu za Watanzania kwa mamilioni. Ni kwa kufikiwa na taarifa za kutisha za mauaji ya mwandishi wa habari. Haya yanaingia katika historia kuwa ni mauaji ya kwanza kwa mwandishi wa habari kufanyika hadharani tangu nchi hii ipate Uhuru. Wengi watakuja kukumbuka walikuwa wapi na walifanya nini siku walipopata taarifa hizo za kutisha. Binafsi, taarifa ile ya mauaji ya Daud Mwangosi siku ile ya Jumapili ya huzuni kwa Taifa ilinikuta nikiwa Iringa Mjini. N umbali wa mwendo wa saa moja kwa gari kufika eneo la tukio, Nyololo, Mufindi. Jioni ile nilikuwa nikifundisha soka ya watoto. Mara baada ya kupata taarifa zile kwa simu, nili

MAHAFALI YA KWANZA IRINGA RETCO BUSINESS COLLEGE

Image
Mh Jaji mstaafu Raymond Mwaikasu akimtunuku Cheti cha Astashahada na Stashahada ya uongozi wa Biashara pamoja na tuzo ya uanafunzi Bora 2010 Beatrice Ndekwa. Wasanii wa kikundi cha Ngoma toka Mkwawa Magic Site wakitumbuiza, 

Waliopanda mbegu DECI hatarini kutolipwa

Image
WATEJA wa Kampuni ya DECI waliopanda mbegu, wanaweza wasilipwe fedha zao, MTANZANIA Jumatatu limebaini. Wateja hao ambao wanaidai kampuni hiyo Sh bilioni 39.27, huenda wasilipwe fedha zao kwa kuwa mchezo wa upatu hautambuliki kisheria. Utata huo ulijulikana mwishoni mwa wiki, baada ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndullu, kuzungumza na MTANZANIA Jumatatu. "Kwanza kabisa, niseme tu kwamba hadi sasa hatujapata nakala ya hukumu hiyo ili kujua inatuelekeza nini kuhusu mchakato wa kuwalipa hao waliopanda mbegu. "Tukipata hukumu hiyo, ndiyo tutaisoma na kufahamu tumepewa jukumu gani na gharama zitalipwa na nani katika kutekeleza mchakato huo. "Sisi tunataka tujue hiyo hukumu inamaanisha nini, maana kwa kawaida anayechezesha na anayecheza upatu wote wana makosa, sasa utamlipaje aliyecheza? "Lakini, kwa kuwa hatujaiona hiyo hukumu, hatujui imetuelekeza nini, lakini i

LAPF KUTUMIA BILIONI 35 UJENZI WA KITUO CHA MABASI MSAMVU

Image
Na Fatma Salum na Hassan Silayo- MAELEZO Mfuko wa pensheni wa LAPF unatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 35 katika mradi wa kituo cha mabasi eneo la msamvu Mkoani Morogoro. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja wa mfuko huo Kanda ya Mashariki Sayi Lulyalya alisema mradi huo ambao ni ubia kati ya Manispaa ya Morogoro na mfuko wa LAPF unatarajiwa kuanza wakati wowote mwaka huu. Sayi alisema hatua za awali za utekelezaji wa mradi huo ambao utakamilika baada ya miezi 18 zimeshaanza kwa kuzungushia uzio katika eneo la ujenzi wa kituo hicho. "LAPF imeamua kutenga takriban bilioni 35 za ujenzi wa kituo cha Msamvu na tunashukuru uongozi wa Manispaa ya Morogoro kwa kutoa eneo la kutosha kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho na michoro imeshakamilika na shughuli za zabuni zinaendelea." Alisema Sayi. Aidha Sayi aliongeza kuwa mradi huo wa uwekezaji utahusisha ujenzi wa hoteli yenye

DIAMOND ATUHUMIWA KUIBA WIMBO WA DYNA..."MY NUMBER ONE"

Image
 Baada ya tuhuma za kuiba wimbo wa H.Baba na Pasha,Msanii Naseeb Abdul Diamond Platnum, ameingia tena ndani ya tuhuma nzito  baada ya  madai   kwamba wimbo anaotaka kuuachia wa No.1 ni wa Dayna. Inasemekana awali Dayna alimtaka Diamond wakafanye wimbo kwa Shedy, Diamond akakubali, akaskiliza mdundo na kumuahidi Dayna kwamba wangefanya wote. Lakini baadae Diamond akamrubuni Shedy na kumwambia ile bit ampe na aachane na kazi ya Dayna. Hii ni demo ya wimbo wa Dayna ambao unafanana kila kitu na wimbo wa Diamond anaotaka kuachia.

MWANAUME ANYWESHWA VIROBA NA "KULIWA JICHO" ( KABAANG) BAADA YA KULEWA

Image
JESHI la Polisi mkoani Singida linamtafuta kijana mmoja mkazi wa Kibaoni katika manispaa hiyo kwa tuhuma za kumlawiti mwenzake na kumharibu vibaya sehemu za haja kubwa baada ya kumnunulia pombe kali aina ya viroba jogoo tisa.   Kamanda wa polisi mkoani hapa, Geofrey Kamwela, alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 3:00 usiku eneo la soko la Kibaoni, kata ya Kindai, na kumtaja mtuhumiwa huyo kwa jina moja la Athuman.   Alisema kuwa baada ya kila mmoja kumaliza kunywa viroba vyake, kijana aliyelawitiwa (jina tunalihifadhi) alimweleza mtuhumiwa kuwa amelewa kupindukia na hivyo kila mmoja arejee nyumbani kwao.   “Walipofika eneo la soko la Kindai, muathirika alimwambia mtuhumiwa amwache hapo ili apumzike kwa vile pombe ilikuwa imemzidi sana lakini ghafla alianguka chini na kisha na kupoteza fahamu,” alisema.   Baada ya muathirika kupoteza fahamu, mtuhumiwa alitumia fursa hiyo na kuanza kumwingilia kimwili kinyume cha maumbile.   Alisema kuwa

CHADEMA WAMKANA AFANDE SELE....WADAI HAWAJAWAHI MUOMBA AGOMBEE UBUNGE MOROGORO..!!

Image
Gazeti la Habari Leo la siku ya leo tarehe 2 Septemba lenye kichwa cha habari "Chadema kuzoa wasanii mastaa" pamoja na mambo mengine, mwandishi amemnukuu mmoja wa wasanii toka mkoa wa Morogoro akisema amewahi kuombwa na viongozi wa mkoa wa CHADEMA kugombea Ubunge. NAOMBA KUWEKA KUMBUKUMBU SAHIHI. 1. Mimi ndiye mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Morogoro, ninayeongo za Baraza la Uongoz la mkoa lenye wajumbe wa5 tu tangu mwaka 2009. 2. Katika vikao vyetu vyote hukujawahi kuwepo kwa AGENDA ya kumuomba/ kumshawishi mtu yeyote kugombea nafasi yoyote. 3. Hatujawahi kumuomba Afande Sele kugombea. Mbali na hilo hatujawahi hata kumuomba tu kujiunga na CHADEMA.     4. Kwa upande wa gazeti la Habari leo, naungana na kauli ya JB kwamba, kuna dalili za wazi kwamba habari hii imepikwa na mwandishi mwenyewe. Asanteni Makamanda. PUUZENI TAARIFA HII Susan Limbweni Kiwanga

NELSON MANDELA ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI

Image
RAIS wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela (95), jana aliondolewa hospitali na kurejeshwa nyumbani ambako ataendelea na matibabu ya maradhi ya mapafu.  Hata hivyo, taarifa ya Serikali ya Afrika Kusini imesema uamuzi huo hauna maana kwamba Mandela amepata nafuu kwa vile hali yake bado ni mbaya na wakati mwingine hudorora zaidi. Taarifa hiyo imeongeza timu ya madaktari wa Mandela inaamini ataendelea kupata matibabu katika makazi yake mjini Houghton kwa kiwango sawa na anayopata akiwa hospitalini mjini Pretoria. Tangazo hilo limekuja siku moja tu baada ya maofisa wa serikali kukanusha ripoti kuwa shujaa huyo wa taifa hilo, alisharuhusiwa. Mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel aliyekuwa amelazwa hospitali tangu Juni 8, mwaka huu anaheshimiwa duniani kwa kuongoza mapambano dhidi ya utawala wa kibaguzi wa wazungu wachache na kuhubiri upatanisho na maridhiano na jamii za weupe pamoja na kufungwa miaka 27 jela. “Timu ya madaktari imetuhakikishia kuwa Mandela ata