Hapa na Pale: Hii ndiyo Mistari ya Nuh Mziwanda Alipokuwa Anamtongoza Wema Sepetu, Utavunja Mbavu
Nuh Mziwanda amejikuta akiumbuka vibaya baada ya Wema Sepetu kuvujisha sauti anayosikika akimtongoza mrembo huyo. Mazungumzo hayo yanachekesha sana hasa kutokana na mistari anayompa Miss Tanzania huyo wa zamani. Haya ni maongezi yaliyofanyika mwezi June (siku moja kabla ya KTMA 2015). Tunafahamu wapo wasioweza kusikiliza clip yote hivyo tumekuandikia mazungumzo hayo. Nuh Mziwanda: Kuna ua moja lilikuwa limefuatwa sana na vipepeo pamoja na nyuki kwaajili ya kutengeneza asali, unanielewa? Wema Sepetu: Yeah Nuh: Kwahiyo lile ua yule mama alikuwa anapenda sana kulitunza na kulifanya special kuliko maua yote. Mama yupo radhi maua yote yakauke lakini lile ua alimwagilie maji ili likue. Wema: Hilo ua lilikuwa nyumbani kwenu? Nuh Mziwanda: Yeah nyumbani kwetu Ilala Posta, alipokulia Shetta kwa akina Shetta pale kwetu hapa. Ua hilo hadi leo hii lipo. Ua ambalo mama analipenda na kulithamini kwakuwa lililikuwa linavutia. Kwahiyo katika kuvutia kwake, vipepeo ...