Posts

Showing posts from December 1, 2013

TANZANIA YAZIDI KUPETA TUSKER PROJECT FAME

Image
  Mshiriki toka Tanzania anayetuwakilisha kwenye mashindano ya Tusker project fame amefanikiwa kusonga mbele kwa mara nyingine baada ya kuwa kikaangoni  yeye pamoja na washiriki wenzake wote ndani ya Tusker project fame.Waliotoka wiki hiii ni Phiona toka Rwanda na Kojjo kutoka Uganda.Hongera hisia Tanzania Gooooooooooooooooo Goooooooo

Taarifa ya kusimamishwa uongozi kwa Mwenyekiti wa CHADEMA wilayani Monduli

Image
TAARIFA KWA UMMA Kwa niaba ya baraza la uongozi la mkoa wa Arusha, napenda kuujulisha umma wote kwa ujumla kuwa mwenyekiti wa wilaya ya monduli Mchungaji Amani Silanga Mollel amekoma/amesimamishwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya monduli kuanzia tarehe 29 Novemba 2013 kufuatia tuhuma nzito za uvunjifu wa kanuni za maadili ya chama.  Hatua hii imefikiwa baada ya kuthibitika na yeyé mwenyewe kukiri mbele ya kikao cha kamati tendaji ya wilaya ya monduli kilichoketi tarehe 29 Novemba 2013 saa NNE asubuhi kuwa alitoa tamko batili akitumia wadhifa wa mwenyekiti wa wilaya bila ridhaa ya kamati tendaji na huku akidanganya kuwa ni tamko kwa niaba ya wilaya ya monduli.  Katika tamko lake ametoa tuhuma dhidi ya wajumbe wa kamati kuu na viongozi wakuu wa kitaifa kwa maamuzi halali ya kikao cha kamati kuu huku akijua kuwa anavunja kanuni za chama kwa mujibu wa katiba ya chama toleo la mwaka

Mwigizaji PAUL WALKER wa Marekani afariki dunia kwenye ajali mbaya ya gari. Ni yule wa filamu Fast and Furious

Image
Muigizaji Paul Walker , anayejulikana  sana duniani kwenye uigizaji kupitia filamu za Fast and Furious , amefariki katika ajali ya gari. Ajali hiyo imetokea katika eneo la Santa Clarita, k askazini ya Los Angeles wakati alipokuwa katika tukio la kijamii. Walker alikuwa ni abiria katika gari aina ya  Porsche kwamba waliopotea kudhibiti na kugonga ama taa ya posta au mti kabla ya kupasuka ndani ya moto . Kifo muigizaji baadaye kilithibitisha  kwenye ukurasa wake wa Facebook  . Taarifa kwenye  ukurasa huo  zilisema:  " kwa moyo  mnzito kwamba tunapenda kuthibitisha kwamba Paulo Walker amefariki leo katika kutisha ajali ya gari wakati akienda kuhudhuria tukio upendo kwa shirika lake kuwasaidia watu duniani kote. "Yeye alikuwa ni abiria katika gari ya rafiki yake, ambayo wote walipoteza maisha yao . "Asante kwa ajili ya kuweka familia yake na marafiki katika maombi yako katika wakati huu mgumu sana . RIP Paul Walker

KATIBU WA CHADEMA WILAYA YA CHUNYA AJIUNGA NA CCM

Image
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahmani Kinana akifafanua jambo wakati alipokuwa akiuliza swali alipokagua ujenzi wa barabara ya Mbeya Chunya yenye kilomita 36 inayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 56 za kitanzania , Barabara hiyo inajengwa na kampuni ya kichina ya China Communication Construction Company, Kinana yuko katika ziara ya kikzani ya mikoa mitatu Ruvuma, Mbeya na Njombe akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kiamataifa leo amemaliza ziara katika jimbo la Lupa na kesho anaendelea na ziara katika jombo la Songwe wilayani China, kulia ni Mh. Abbas Kandoro Mkuu wa mkoa wa Mbeya na katikati ni Dr. Asha Rose Migiro.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-LUPA-CHUNYA) Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahmani Kinana akipiga makofi wakati Braison Mwasimba aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA

ONA MATUKIO ZAIDI 200 YA KILICHOJILI KATIKA FAINALI ZA EBSS 2013 ... ILIKUWA NI BALAA

Image
    Mshindi wa EBBS 2013 Emmanuel Msuya.                 Mwanamuziki Snura Mushi akiwajibika jukwaani kwa kucheza wimbo wake wa 'Nimevurugwa'.… Mwanamuziki Snura Mushi akiwajibika jukwaani kwa kucheza wimbo wake wa 'Nimevurugwa'. Mwanamuziki Walter Chilambo ambaye ndiye mshindi wa shindano la EBSS 2012 akitumbuiza stejini

MTU MMOJA AKUTWA NA BUNDUKI PAMOJA NA RISASI 13 JIJINI ARUSHA

Image
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas akiwaonyesha waandishi wa habari (Hawapo pichani) bunduki aina ya shortgun iliyokutwa nyumbani kwa mtu anayejulikana kwa jina na Jumanne Abdallah Maarufu kwa jina la Babu G (25) Unga Ltd jijini hapa ambaye anatuhumiwa kuhusika katika matukio mbalimbali ya ujambazi hapa nchini. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha) Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas akionyesha risasi zilizokutwa nyumbani kwa mtuhumiwa wa ujambazi Jumanne Abdallah maarufu kwa jina la Babu G maeneo ya Unga Ltd jijini hapa. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha) Na Rashid Nchimbiwa Jeshi la PolisiArusha Mtu mmoja anayetuhumiwa kwa ujambazi ajulikanaye kwa jina la Jumanne Abdallah Maarufu kwa jina la Babu G (25) Mkazi wa Unga Limited jijini hapa amekamatwa na Jeshi la Polisi akiwa na bunduki aina ya short gun pamoja n

Hivi ndivyo Emmanuel Msuya alivyozoa Milioni 50 za Ebss ... Mpango mzima upo hapa kuanzia Red Carpet mpaka kukabidhiwa zawadi

Image
Kinyanganyiro cha kumtafuta Super Star wa Bongo kupitia Epiq Bongo Star Search 2013 kimekamilika alfajiri hii kwenye ukumbi wa Escape 1. Mashindano haya ambayo kidogo yalichelewa kuanza yalipambwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Barnaba,Makomando,Young Killer,water chilambo,Shaa,Kimbunga na Snura. Katika mashindano haya ambayo yalikua na jumla ya washiriki watano  ambao ni Amina Chibaba,Elizabeth Mwakijambile,Emmanuel Msuya,Maina Thadei na Melisa John,ambao walipita kwa round tatu kisha majaji kuwapunguza watatu na kisha kubakia Emanuel Msuya na Elizabeth Mwakijambile katika Round ya 4 na ya mwisho. Katika round ya mwisho,Emmanuel Msuya ameibuka kidedea na kuwa Mshindi wa Epiq Bongo Star Search 2013,akiwa ni mshiriki anaetokea Jijini Mwanza na kumpokea taji water chilambo ambae alikua mshindi wa mwaka jana. Zawadi kwa mshindi wa mwaka huu ni Milion hamsini[50]ambayo kakabidhiwa jukwaani. Hiki ndicho kinachoendelea kwa sasa,upande wa redcarpet

PENNY ASUMBULIWA NA GONJWA LA AJABU, APUNGUA GHAFLA

Image
MTANGAZAJI wa Runinga ya DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’ ameamua kujikondesha mwili ambapo amefanikiwa kupoteze uzito usiopungua kilo  18 mwilini. Akizungumza na Weekly Star Exclusive, Penny alifunguka kuwa, kutokana na kuona mwili wake unavimbiana, aliamua kufanya mazoezi maalum ya kupunguza mwili sambamba na kufanya ‘dayati’ ambayo imembadilisha muonekano wake (tazama picha ndogo). “Nimeamua tu kuubadilisha muonekano wangu wa unene kwani nilikuwa ninazidi kuwa bonge, kweli nimefanikiwa maana hata uzito nimepungua kwa sasa. “Kabla sijaanza kufanya mazoezi nilikuwa na kilo 85 lakini sasa nimepungua hadi kufikia kilo 67, ni mafanikio makubwa ambayo nimeyapata katika zoezi langu la kupunguza uzito,” alisema Penny ambaye ni ‘ubavu’ wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’. Kuhusu msosi, kwa sasa Penny asubuhi anakula ‘ma-apple’ mawili au kipande cha papai, mchana anakunywa juisi na usiku anamalizia na saladi ya samaki au kuku, analala.

SUPER STAR SINGER TID ATUPWA RUMANDE TENA. KISA HIKI HAPA .... !!

Image
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Khaleed Mohamed 'TID' yupo mahabusu katika Kituo cha Polisi Oysterbay tangu jana usiku baada ya kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi msichana anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake,  Mariam Nnauye.  Huyu Ndio Mariam Nnauye. Taarifa zinasema kuwa ugomvi ulianza maisha club jana usiku baada ya TID kumkuta Mpenzi wake akiongea na mwanaume mwingine bila ruhusa ya Top In Dar na ndio Top akamvuta mpenzi wake na kumpiga makofi.Bila kijali mapenzi yao binti huyo alikwenda moja kwa moja kituo cha polici Osterbay na kutoa taarifa ya kupigwa naTid. Tid ametoka mida ya saa tano asubuhi kwa Dhamana na ataripoti tena polici jumatatu.   Source: Sam Misago

MWANAMUZIKI TABU LEY AFARIKI DUNIA

Image
l Mwanamuziki mkongwe wa Congo, Pascal Tabu Ley Rochereau amefariki dunia leo asubuhi baada ya kulazwa katika hospitali ya nchini Ubelgiji. Kwa mujibu wa mwanae Charles Tabu, aliyeongea na Radio Okapi, Tabu Ley amefariki kwa kiharusi na Kisukari. Naye Nyboma Mwandido, mwanamuziki mwenzie aishiye jijini Paris, Ufaransa amethibitisha kifo cha msanii huyo kilichotokea leo Jumamosi saa 2 asubuhi Brussels. Tabu Ley alikuwa mgonjwa mahututi kwenye hospitali hiyo kutokana na kusumbuliwa na kiharusi alichokipata mwaka 2008. Kiharusi (stroke) kilimfanya awe kwenye kiti cha walemavu tangu muda huo. Pamoja na muziki, Tabu Ley aliwahi kuteuliwa kuwa waziri na Rais Laurent Kabila mwaka 1997 na baadaye kuwa mbunge. Awali, msanii huyo wa Rhumba aliyekataa kuwa mshairi wa Rais Mobutu Sese Seko alilazimika kuikimbia nchi hiyo. Miaka ya mwishoni alikuwa akiishi Paris, Ufaransa akipata matibabu kabla ya hivi karibuni kupelekwa Ubelgiji kupata matibabu maalum. Katika