Njemba Amchezea Sharubu JPM, Adaiwa Kumweka Kinyumba Denti Form 2
Denti huyo baada ya kunaswa chumbani. NJEMBA aliyetajwa kwa jina moja la Sadick anadaiwa kumweka kinyumba denti wa kidato cha pili (jina la mwanafunzi na shule vinahifadhiwa), jambo lililotafsiriwa kuwa ni kuwachezea sharubu viongozi wa ngazi ya juu kabisa nchini akiwemo Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ ambaye ni hivi karibuni tu ameonya na kutaka zichukuliwe hatua kali kwa wanaojihusisha na mchezo wa mapenzi na wanafunzi. ONYO LA RAIS Rais Magufuli alitoa onyo hilo alipokuwa akizindua Barabara ya Bagamoyo-Msata, mkoani Pwani, mwezi uliopita na kuongeza kwamba serikali yake haitagharamia mwanafunzi aliyepata mimba shuleni. Mwenyekiti wa Mtaa, Adil Omar akiwa na denti. ONYO LA WAZIRI MKUU Mbali na Rais Magufuli, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, akikabidhi vifaa vya maabara kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum hivi karibuni Lugalo jijini Dar alishindilia msumari kwenye onyo hilo, akisema kuwa, yeye pamoja na rais watalala mbel...