Mama Diamond Atoa Siri ya Zari

Mama mzazi wa staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul āDiamond Platnumzā, Sanura Kassim āSandraā ametoboa siri ya mkaza mwanaye, Zarinah Hassan āZari The Boss Ladyā kushindwa kuishi Bongo na badala yake kukimbilia nchini Afrika Kusini āSauzā. Sandra au Mama D aliyasema hayo katika mahojiano maalum na Ijumaa Wikienda juu ya uhusiano wake na Zari kufuatia tetesi kuwa hawaivi ndipo akaweka mambo sawa. Mama D alisema kuwa yeye na Zari wapo vizuri lakini kinachomfanya mkwewe huyo kushindwa kuishi naye Bongo ni kutokana na biashara zake kudoda nchini Afrika Kusini. āUnajua anapokuwa huku (Bongo), biashara zake huwa zinayumba sana, wakati mwingine akipiga simu akiulizia biashara zinakwendaje anaambiwa hali ni mbaya au hazijaingiza chochote hapo ndipo huwa anachanganyikiwa. āKwa mfano hivi karibuni alipiga simu akaambiwa hakuna fedha kabisa na biashara haziendi. Kilichofuata ni kujiandaa na kumchukua Tiffah (Latifah Nasibu) kisha akaondoka zake. āHicho ndicho kinacho...