MUUZA CHIPS AMTEKA MTOTO TANDALE DAR NA KUTOKOMEA NAE KUSIKOJULIKANA
MTOTO wa kike mwenye umri wa miaka mitatu, Maryment Ibrahim ambaye anaishi Tandale jijini Dar es Salaam, hivi karibuni alipatwa na masahibu makubwa baada ya kutekwa nyara na kutoroshwa hadi Gairo mkoani Morogoro huku mtekaji akidaiwa kutaka apewe shilingi milioni 6 ili amuachie. Mama mzazi wa mtoto aliyetekwa akiwa na mwanaye. Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Oktoba 16 mwaka huu baada ya kijana mmoja, anayefanya biashara ya kuuza chipsi anayejulikana kwa jina la Issa Ramadhani, kudaiwa kumchukua mtoto huyo aliyekuwa akicheza nyumbani kwao na kutoweka naye kabla ya wazazi wake kubaini na kwenda kutoa taarifa kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’. Awali, ilidaiwa Ramadhan alikuwa na tabia ya kuwachukua watoto wadogo wa mtaani hapo na kuondoka nao na kuwarudisha baadaye, kitu kilichowafanya wazazi wa mtoto huyo kutokuwa na wasiwasi. Mtuhumiwa wa utekaji. Wakizungumza na mwandishi wetu, wazazi wa mtoto huyo walisema waliamua kutoa taarifa polisi na ...