Posts

Showing posts from July 22, 2013

Maalim Seif atembelea wagonjwa , afuturu nao

Image
Wananchi mbali mbali wakijumuika katika futari iliyoandaliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, nyumbani kwake Mbweni Zanzibar.     Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akimjuilia hali  na kumfariji Bi. Mkasi Jihadi wa Kijini Makunduchi wakati wa ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika  Mkoa wa Kusini Unguja.   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na wananchi wa Makunduchi wakati wa ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika  Mkoa wa Kusini Unguja. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akimjuilia hali na kumfariji mzee Muombwa Rashid wa Kajengwa Makunduchi, wakati wa ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika Mkoa wa Kusini Unguja. (picha na Salmin Said, OMKR). Na Hassan Hamad OMKR Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif H...

MASHEIKH DAR WAMKINGIA KIFUAA LOWASSA

Image
TAASISI ya Amani ya Kiislamu (TIPF), imewapongeza viongozi mbalimbali akiwamo Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kutokana na michango yao ya maendeleo katika jamii. Taasisi hiyo imempongeza Lowassa kutokana na jitihada zake za kuendesha harambee iliyowezesha kukusanywa Sh milioni 520, kwa ajili ya kuchangia redio ya kiislamu ya Mkoa wa Mwanza, IQRA FM.   Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Sheikh Sadiki Godigodi, alisema viongozi wa aina hiyo ni mfano wa kuigwa na kupigiwa mfano. “Tunampongeza kwa kuwa ni jambo kubwa sana na zito alilolifanya kwa maendeleo ya dini yetu, kwani redio hiyo itasaidia kutoa elimu ya dini na hofu ya Mungu katika jamii. “Viongozi wa aina hii wasiokuwa na ubaguzi wa dini katika kuchangia maendeleo ni mfano mzuri, hatuwezi kuwavunja moyo kwa kuwabeza, jamii inapaswa kutambua mchango wao.  Mwingine hapa ni Mwenyekiti mtendaji wa IPP, Reg...

MENEJA KAMPENI WA MWENYEKITI WA CHADEMA-MBOWE AHAMIA CCM

Image
Mchungaji Simboni, aliyekuwa Meneja wa Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai, Mh. Mbowe na Katibu wa Chadema Wilaya ya Hai akirudisha kadi yake ya Chadema jana kwa Mwenyekiti wa Wazazi/CCM Taifa Mh. Bulembo jana kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Kaway, Longilo Wilaya ya Hai. Mchungaji Simbon alitangaza rasmi kurejea CCM, alipokuwa zamani. CHANZO:Jamiiforum/jukwaa la siasa 

SHILOLE ATANGAZA BIFU LA NGUMI BAADA YA SINTAH KUMPONDA KUWA ANAUWEZO MDOGO KIMUZIKI

Image
MWIGIZAJI wa kike wa filamu na muziki Bongo zuwena Mohamed ‘Shilole’ amemtangazia hali ya hatari msanii mwenzake wa filamu na mtangazaji wa televisheni Christina John ‘ Sintah’ kuwa p opote atakapomkuta lazima amchape kwa kipigo ambacho hatasahau katika maisha yake ... Shilole  ametoa kauli hiyo kufuatia kuandikwa na mwanadada huyo katika mtandao wake akimbeza kwa kejeli. . “Ni kweli sisi wanawake hatupendani na kuwa na wivu wa kijinga, mtu anakurupuka anakotoka bila hata kufanya utafiti na kunibeza eti sina uwezo wa kuimba na JLO (Jenifer Lopez) .... "Kuna mtu aliyetegemea mimi kwenda kufanya show Marekeni! Sasa ninachomwambia ninamtafuta nikikutana naye nimtapa kipigo cha Mbwa mwizi,” aliongea kwa hasira Shilole. Katika mtandao wake Sintah aliandika kwa kusema Shilole ni sawa na mtu anayeota ndoto za mchana, na kumkejeli kwa kusema kuwa aendelee kuota anaweza baadae kurudi katika hali yake...   Sehemu ya maneno yanayomkera Shilole ni haya:...

LINAH AKANUSHA MADAI YA KUBAKWA USIKU BAADA YA KULEWA

Image
Mrembo na mwanamuziki wa kike nchini, Linah Sanga amezikanusha ripoti zilizosambazwa leo kuwa amebakwa na rapper Kimbunga na kudai kuwa ameshangazwa mno na taarifa hizo. Taarifa hizo zimeanza kusambazwa leo mchana baada ya akaunti ya Facebook inayoonekana kuwa ya rapper Kalapina yenye jina ‘KalApina Kikosi Cha Mizinga’ kuandika:   “Mtoto kimbunga amechamba ana leta usela mavi mambo ya kizamani hivi yupo chini ya ulinzi osterbay police kwa kosa la kumbaka msanii lina.” Mwandishi wetu amezungumza na Linah ambaye amesema amepigiwa simu na watu wengi wa karibu kumuuliza suala hilo wakiwemo, Barnaba, Ditto, Amini na mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown.   Amesema Soudy alimwambia kuwa ameziona taarifa hizo kwenye Facebook kwenye akaunti ya Kalapina. “Sasa nikasema Kalapina ameandika hivi, kwasababu sijaingia mwenyewe kuangalia chochote.  "Sikutaka kujipa stress kwasababu kuna kazi nafanya nisije nikaharibu kazi kwahiyo nikaona vitu vin...

MAJUNGU YAWAFANYA "SCORPION GIRLS" WAZINGUANE

Image
MEMBA wa Kundi la Scorpion Girls, Isabela Mpanda ‘Bela’ na Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ wametofautiana hadi kufi kia hatua ya kutukanana na kutupiana nguo nje.   Mpango mzima ulitokea hivi karibuni Kijitonyama jijini Dar, nyumbani kwa Isabela ambapo chanzo cha ugomvi huo ni baada ya Isabela kumsifi a mtandaoni X-memba wa kundi lao, Jacqueline Pentezel ‘Jack wa Chuz’ kwa kununua gari, ndipo Kabula  alipokasirika na kuanza kumtukana Bela na mama yake matusi ya nguoni.   “Sikumuelewa kabisa Jini, kumsifi a Jack kuhusu kumiliki gari ndiyo kumemfanya anitukane? Iliniuma sana na sitamsamehe, bora kila mtu achukue hamsini zake, nguo zake nilimtupia nje,” alisema Bela na kusisitiza kufanya muziki peke yake kwa sasa.

WATOTO WAWILI WABAKWA NA BABA ZAO JIJINI DAR

Image
Ukatili wa kutisha umewakuta watoto wawili wa familia tofauti wakidaiwa kubakwa na wazazi wao huku mmoja akifanyiwa unyama huo na baba yake mzazi na mwingine baba yake mdogo. Habari zilizopatikana kutoka kwa ndugu, wazazi na majirani wa watoto hao zilisema kuwa wote walifanyiwa ukatili huo siku moja kwa nyakati na mazingira tofauti wilayani Temeke, Dar hivi karibuni. Watoto hao ambao wote walifikishwa siku moja katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke kwa matibabu, walieleza jinsi walivyotendewa unyama huo wa kusikitisha ambao mzazi au mlezi hapaswi kumtendea mwanaye. Wakwanza ni Anifa (8) ambaye alieleza kuwa alibakwa na baba yake mdogo aliyemtaja kwa jina moja la Amani. Wapili ni Prisca ambaye alimweleza mwanahabari wetu kuwa alibakwa na baba yake mzazi aliyemtaja kwa jina moja la Charles. Wakizungumza na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti wakiwa wodini hospitalini hapo wakiuguzwa majeraha, watoto hao waliokuwa sambamba na mama zao, walieleza kwa kina kile wali...

ASKARI WA JWTZ WALIOUAWA DARFUR KUAGWA LEO MAKAO MAKUU YA JESHI

Image
Askari saba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), waliouawa katika jimbo la Darfur nchini Sudan, wanatarajiwa kuagwa leo kwenye viwanja vya makao makuu ya jeshi hilo. Miili ya wanajeshi hao iliwasili nchini juzi kwa ndege maalumu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J. K Nyerere, Terminal One na kwenda kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Lugalo jijini Dar es Salaam. Wanajeshi waliouawa ni Sajenti Shaibu Othuman, Koplo Oswald Chaula, Koplo Mohamed Juma, Koplo Mohamed Chikilizo, Rodney Ndunguru, Peter Werema na Fortunatus Msofe. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano, Makao Makuu ya JWTZ, ilieleza kuwa askari hao wataagwa leo na shughuli hiyo itahudhuriwa na familia, makamanda wa jeshi na viongozi wa Serikali.   “Shughuli ya kuaga kwa heshima za kijeshi itaanza saa tatu kamili asubuhi katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Upanga na itaendelea mpaka mchana kab...