Posts

Showing posts from May 2, 2016

Watahiniwa 75,000 Waanza Mtihani wa Kidato cha Sita Leo

Image
Watahiniwa  74,920 leo wanaanza kufanya mtihani wa kuhitimu Kidato cha Sita katika shule mbalimbali nchini huku watahiniwa 11,597 wakifanya mtihani wa Ualimu. Ofisa Habari wa Baraza la Mitihani (NECTA), John Nchimbi amesema kuwa mtihani wa kidato cha sita unaanza leo hadi Mei 19, mwaka huu. Nchimbi amesema kati ya watahiniwa hao waliosajiliwa, watahiniwa 65,610 ni watahiniwa wa Shule huku watahiniwa wa Kujitegemea wakiwa 9,310. “Kati ya watahiniwa wa shule 65, 610, watahiniwa wasichana ni 24,549 na wavulana ni 41,061 huku watahiniwa wa kujitegemea wasichana wakiwa ni 3,176 na wavulana ni 6,134,” alisema Nchimbi. Kwa upande wa mtihani wa ualimu, Nchimbi amesema kati ya watahiniwa 11,597 watakaofanya, watahiniwa 10,942 wanafanya Ualimu Daraja A na watahiniwa 654 wanafanya mtihani wa Stashahada ya Sekondari na mmoja anafanya Stashahada ya Ufundi.   “NECTA inatoa mwito kwa kamati za mitihani za mikoa, na wilaya kuhakikisha kuwa taratibu zo...

Mahakama ya Kisutu Yatoa Hati ya Kukamatwa kwa Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob

Image
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar imetoa hati ya kukamatwa kwa Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob (Pichani)kutokana na kutofika mahakamani. Meya huyo anakabiliwa na shitaka la kumshambulia  mwandishi wa Habari wa gazeti la Uhuru, Christopher Lissa na kumsababishia maumivu makali. Kesi hiyo jana ililetwa mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa kwa ajili ya usikilizwaji ambapo upande wa mashitaka ulikuwa na shahidi mmoja. Wakili wa serikali Onolina Mushi alidai kwamba,kesi hiyo ililetwa kusikilizwa lakini mshitakiwa pamoja na wakili wake hawajafika mahakamani. Kutokana na hali hiyo,aliiomba mahakama itoe hati ya kukamatwa kwa mshitakiwa huyo pamoja na kupanga tarehe nyingine ya kuendelea kusikiliza shauri hilo. Hakimu alikubali maombi hayo ikiwemo ya kutolewa hati ya kukamatwa kwa Meya huyo.Kesi hiyo iliahirishwa hadi Mei 23 mwaka huu kwa ajili ya usikilizwaji. Katika kesi hiyo,Boniface anadaiwa kutenda kosa hilo  Septemba 11, mwaka jan...

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI MJINI DODOMA

Image
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo Mei 2, 2016  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiendesha kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo Mei 2, 2016.PICHA NA IKULU.