KUSAIDIA JAMII KWAMPA CHETI CHA HESHIMA MAMA KIKWETE
Na Anna Nkinda – Brussels, Ubelgiji Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amepewa cheti na Umoja wa wake wa Mabalozi wa Afrika waishio katika nchi za Jumuia ya Ulaya kwa kutambua na kuthamini mchango wake na kazi anazozifanya za kuwasaidia wanawake, wasichana na watoto wa Tanzania. Cheti hicho amekabidhiwa jana katika hafla fupi ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na wake hao wa mabalozi katika ukumbi wa mikutano uliopo Hoteli ya Sheraton mjini Brussels. Mama Kikwete ni mmoja kati ya wake wa Marais wa tano wa Afrika waliokabidhiwa vyeti hivyo vya heshima kutokana na kazi zao wanazozifanya za kuisaidia jamii na kuhakikisha kuwa inapata mahitaji ya muhimu kama huduma ya afya na elimu. Akiongea kabla ya kuwakabidhi wake hao wa marais vyeti hivyo Mke wa Balozi wa Equatorial Guinea ambaye pia ni rais wa umoja huo Mama Mangue de Nvono Nca alisema nia ya kuanzishwa kwa umoja wao ni kulitambulisha bara la Afrika ambalo linajulikana kuwa na changamoto za nja