Posts

Showing posts from November 12, 2015

MBASHA LIVE NA KIFAA

Image
Richard Bukos CHA KUFIA! Msanii wa muziki wa Injili Bongo, Emmanuel Mbasha, Alhamisi iliyopita alinaswa kwenye maongezi yaliyoambatana na pozi lenye maswali kwa kuonekana akichukua namba fastafasta kwa mrembo ‘kifaa’. Wakifurahia jambo. Mbasha alinaswa na kifaa hicho ndani ya Viwanja vya Ikulu jijini Dar ambapo kulikuwa na hafla ya kumpongeza Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Pombe Magufuli baada ya kuapishwa kushika nafasi hiyo. Katika tukio hilo, wawili hao walikuwa kwenye kona wakitafuna vipapatio vya kuku na kubadilishana mawazo huku kila mmoja akimuonesha mwenzake tabasamu la amani na upendo.‘Wapiga chabo’ waliowaona walifika mbali zaidi kwa kusema eti, Mbasha akiishi na kifaa hicho watapendezana kwani anafanana na mkewe waliyetengana, Flora. Akizungumza na Amani kuhusu mdada huyo, Mbasha alisema ni shabiki wa kazi zake na hana mpango wa kuziba nafasi ya Flora.

SHAMSA: BORA NIFE KULIKO KURUDIANA NA MUME WANGU

Image
Imelda Mtema MAKUBWA!! Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Shamsa Ford ameibuka na kukataa katakata kurudiana na aliyekuwa mumewe, Dickson Matoke ‘Dick’ akisema kuwa kama watarudiana basi atakuwa ameshafariki dunia au bora afe kuliko kurudiana naye. Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Shamsa Ford. Shamsa aliyasema hayo juzikati baada ya kuulizwa na Amani kama ana mpango wa kurudiana na mumewe huyo ambapo alisema licha ya kuzaa mtoto mmoja (Terry) na mwanaume huyo, lakini katika maisha yake hafikirii kamwe kurudiana naye huku akasisitiza kuwa, kwa sasa ana maisha yake mengine. “Mimi nirudiane na Dick? Labda niwe nimekufa na ni bora nife kuliko kurudiana na Dick. Ujue sasa hivi nina thamani kubwa zaidi na nipo na mtu ambaye ananipenda, nampenda,” alisema Shamsa.Hivi karibuni, Dick aliripotiwa na gazeti moja la Global akisema bado anampenda sana Shamsha na yuko tayari kurudiana naye baada ya kumwagana.

KIMENUKA CHADEMA: MBOWE APEWA SIKU TATU KUTENGUA UTEUZI WA MBUNGE WA VITI MAALUM

Image
BAWACHA Mkoani Ruvuma wampa Mwenyekiti Mbowe siku tatu kutengua uamuzi wa kumteua Zubeda Sakuru Ubunge Viti Maalum, wasikitishwa na uteuzi huo wadai ni wa upendeleo -Aidha wameshangazwa na uongozi wa Chama kutotokea kwenye kikao maalum cha kupinga uamuzi huo.Wamesema wamesikitishwa kwa chama kuonyesha waziwazi kwamba ni mali ya mtu mmoja na familia yake. Iweje leo waletewe Mbunge wa Viti Maalum kutoka Tanga, hali hajui Mkoa wa Ruvuma ukoje na Jiografia yake. Aidha pia wameshangazwa na uongozi wa Chama hiko kutotokea kwenye kikao maalum cha kupinga uamuzi huo BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

UKAWA KIMENUKA:..JAMES MBATIA AKIONA CHA MOTO MWANZA HAPATOSHI

Image
Viongozi wa chama cha NCCR - MAGEUZI Mwanza inasemekana wamejiuzuli uongozi ndani ya chama chao kwa madai ya M/kiti wa chama hicho James Mbatia kukidhohofisha chama kilichokuwa na wabunge wanne na sasa kina mbunge mmoja. Waliojiuzulu inasemekana ni Kamishina wa mkoa Ramadhan Amran, M/kiti wa jimbo la Nyamagana na Ilemela na Kiongozi wa vijana Nicolas Clinton.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISITAREHE 12.11. 2015

Image